Zile habari za nakupenda, nakupenda pia kila mtu anajua siku hizi na ni
kawaida kwa miaka ya sasa, kuitana baby, hubby,sweet,mpenzi, mahabuba
na majina mengine mengi sio lazima niyataje yote, ila unajua huyo
mahabuba wako hata kama anakupenda vipi kuna vitu hawezi kukwambia
ukweli, kuna vitu katika mahusiano watu huwa wanafichana na hata kama
mnaambiana basi mnadanganyana.
Mahusiano yako ya nyuma
Ni vigumu sana wapenzi kuelezana historia zao za mapenzi hasa inapokuja
swala la umetembea na wangapi? Hapa kama uliambiwa umedanganywa tafiti
zinaonyesha wanaume ndo wanajua kudanganya kwenye swala hili kuliko
wanawake japokuwa kwa asilimia kubwa wapenzi huwa hawaambiani ukweli
kuhusu watu wangapi wameshakuwa na mahusiano nao ya kimapenzi. Kwahiyo
ni bora usiulize usijisumbue.
Kipato
Hapa inakuwa shida kidogo kwani hela haina mapenzi, haina undugu na ni
mara chache ukute wapenzi wanajua mishahara au kipato cha mwenza wake,
wapenzi wengi huwa wanafichana na wengine hata wanadanganya kuhusu
madeni waliyonayo ni kawaida sana kwa mapenzi ya sasa hasa hali ya
kipato ilivyo ngumu.
Kufurahia Tendo
Wapenzi wengi hawaambiani kweli hasa wanapo kutana kimwili, kama
walifurahia au walichukia, wanawake wanasifika kwa kudanganya
wameridhika, ila pia wanaume huwa hawasemi kama msichana hayuko vizuri
kwenye game, na ndo maana watu baada ya kuachana ndo utasikia
wanachafuana oooh wewe ulikuwa kama gogo na mara ooh wewe ulikuwa kama
toothpick mambo kama hayo.
Muonekano
Kuna wakati mtu anapoteza mvuto wake wa asili lakini inakuwa vigumu kwa
wapenzi kuambiana ukweli labda mtu amenenepa sana, au amekuwa na kitambi
sana na hana mvuto lakini sababu ya mapenzi au uoga inakuwa vigumu
wapenzi hawa kuambiana ukweli
Matumizi ya Kilevi
Kwenye matumizi ya pombe baadhi huwa wanakuwa wawazi, lakini wapo
wanaoficha matumizi mengine ya kilevi kama kuvuta sigara na matumizi ya
miraa au mirungi,
Hisia zake kwa mpenzi wa zamani (EX)
Wapo watu wanaingia kwenye mahusiano wakiwa bado wana hisia za mapenzi
na wapenzi wao wa zamani lakini sio rahisi kusema hayo kwa wapenzi
wao,na hata wakiulizwa huwa wanadanganya. Na sio raisi kuleta habari za
mapenzi ya nyuma kwa mpenzi mpya. Ni vigumu kukwambia anavyojisikia
jua ya mpenzi wake wa zamani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment