09 December, 2015

KLAY THOMPSON AWAKUMBUSHA WATU UWEPO WAKE, GOLDEN STATE WARRIORS MOTO CHINI, WASHIKA KALAMU YA NBA.

warr
Ni kama Golden State Warriors wameishikilia kalamu ya NBA. Ni kama Stephen Curry ameiba kamera za waandishi, lakini Klay Thompson alijaribu kuwakumbusha pia sio vyema kumsahau kirahisi vile. Warriors yaendelea kuonyesha sio timu ya kawaida na haibahatishi.
Vyombo vya habari huingia uwanjani vikitizama Curry yupo wapi lakini yeye huingia akitizama naipeleka wapi Golden State Warriors. Ndio maana mchezaji mwenzake akiwa moto haoni shida kumpa show aiendeshe. Ndicho alichofanya kwa Klay Thompson ambaye alimaliza mchezo akifunga pointi 39, rebound 7 na pasi 6 na Warriors wakashinda 131-123 dhidi ya Indiana Pacers.
Kila ukitizama namna Warriors wanavyocheza ni rahisi kuamini kuwa kuvunja rekodi ya Chicago ya kushinda michezo 72 kwa msimu ni jambo linalowezekana kabisa. Klay Thompson alifunga mitupo ya pointi 3 kumi kati ya 16 aliyojaribu. Stephen Curry aliongeza pointi 29, pasi 10 na rebound 7.
Paul George ameendelea kuwa na msimu bora ambapo aliiongoza Pacers kwa kufnga pointi 33, huku C.J Miles akifunga pointi 24.
war
REKODI ZILIZOWEKWA.
Stephen Curry sasa amefunga pointi 3 katika michezo 87 mfululizo, akifikia rekodi ya Rashard Lewis ya msimu wa 2007 mpaka 2009.
Warriors wameendelea kuimarisha rekodi yao bora ya kuanza msimu kwa michezo mingi mfululizo wakifikisha 23 sasa. Warriors pia wameshinda michezo 27 mfululizo ikiwemo 4 ya kumalizia msimu uliopita na sasa wamelingana na MiamiHeat ya msimu wa 2012-13 katika nafasi ya pili. Wamebakisha rekodi ya michezo 33 ya Los Angeles iliyowekwa msimu wa 1971-72.
Golden State Warriors sasa wameshinda michezo 13 mfululizo ya ugenini, ya kufungua msimu.  Wamevunja rekodi ya michezo 12 mfululizo waliyokuwa wamelingana na New York Knicks.
Warriors wamevuka pointi 100 katika michezo yote 23 waliyocheza msimu huu, wamefanya hivyo kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1966-67.
Warriors imekuwa ni timu ya kwanza katika timu zote zinazoshiriki michezo katika mashindano ya michezo yote marekani ikiwemo Hockey, Baseball, American Football na NBA kuwahi kushinda michezo 16 mfululizo katika misimu miwili mfululizo.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...