17 August, 2016

Kenya watwaa medali nyingine ya Dhahabu katika Riadha mita 1500

Kipyegon atwaa Medali ya dhahabu
Kenya imeng'ara tena baada ya mwanariadha wake Faith Kipyegon kunyakua dhahabu ya tatu kwa ajili ya Kenya katika mbio za mita 1500 wanawake.

Kwa upande wa wanaume Mjamaica Omar McLeod naye alinyakua dhahabu ya mita 110 wanaume.
Leo baadaye pia tunategemea kuwaona tena wakenya Kipruto Conseslas, Ezekiel Kemboi na Brimin Kiprop pamoja na Jacob Araptany kutoka Uganda wakishiriki mbio za mita 3000 za kuruka maji na vihunzi.

15 August, 2016

New Audio: Nay Wa Mitego Ft. Tiki - Good Time

Nay wamitego kaachia ngoma yake mpya baada ya kupata misuko-suko ya hapa na pale, mara kufungiwa na mambo kibao.. Ngoma inakwenda kwa jina la Good Time akiwa kamshirikisha msanii anaye julikana kwa jina la Tiki. Bonyeza hapo chini kuupakua wimbo Huo(Mkito)

Sababu ya Chameleone na Diamond Kutofanya Collabo mpaka sasa


Msanii wa mkongwe wa muziki nchini Uganda Jose Chameleone amefunguka na kusema kuwa hana tatizo lolote linalomfanya asifanye kolabo na msanii wa bongo fleva kutoka Tanzania,Diamond kama watu watu wengi wanavyodhani kuwa wana bifu.

Akiongea na mtangazaji wa Kenya,William Tuva wa kipindi cha Mseto,Chameleone amesema kuwa kupishana kwa ratiba yake na Diamond na kila mmoja kuwa busy ndicho kitu hasa kinachofanya kusiwepo na kolabo ya wawili hao
The problem is,he is busy and I am busy lakini tumwombe Mungu tukipata wakati,it is a very simple thing” alisema Chameleone.

CHANZO: SAMMISAGO.COM

Mchezaj Yannick Bolasie asajiliwa rasmi na Club ya Everton

london
Everton imemsajili mchezaji wa kimataifa Yannick Bolasie raia wa Dr Congo anayechezea timu ya Crystal Palace kwa gharama ya paund milioni 25, kwa mkataba wa miaka 5.Bolasie, mwenye umri wa miaka 27, alitumia misimu minne akiwa na timu ya Palace baada ya kujiunga na timu ya Bristol City ya mjini London mwaka 2012.

Amesukuma gozi mara 143 akiwa na timu ya Palacena kufanikiwa kufunga magoli kumi na tatu , na baadaye akabadilika na kuwa kiungo mbadala katika mechi ya mwishoni mwa wiki iliyopita pale timu yake ilipofungwa na West Brom bao moja kwa nunge.
Meneja wa timu ya Palace Alan Pardew alisema baada ya kufungwa bao moja kwa yai tulitambua kuwa moyo na nafsi yake ziko viko mahali kwingine
Bolasie anasema kwamba uamuzi wa kuhamia upande wa Mersey haukuwa wa busara na kuongeza kwamba lakini sasa nimeibukia Everton, kazi haijafanyika bado .Napaswa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kujisikia nimo ndani yake.Niko tayari kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yangu.sio suala la pesa kwa upande wangu ,suala ni kutimiza malengo ya baadaye ya klabu na kule ambako wanatarajia kuifikisha, napenda tu kucheza mpira.
Naye meneja wa timu ya Everton Ronald Koeman anasema kwamba mchezaji huyo Yannick ni mchezaji aliyekuwa anamnyemelea muda mrefu ulio pita kwasababu ni aina ya winga anaye mpenda ,kwanza ana kasi,ana nguvu, na anao uwezo mkubwa wa kucheza katika nafasi mbali mbali hasa mstari wa mbele.

Bolasie ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Everton katika majira haya .
Moja ya majembe hayo yaliyosajiliwa ni pamoja na mlinda mlango Maarten Stekelenburg anatokea timu ya Fulham, Idrissa Gueye kutoka Aston Villa, wakati kiongozi wa timu ya Wales Ashley Williams aliungana na timu hiyo tarehe kumi ya mwezi huu akitokea Swansea kwa ada isiyojulikana, huku ikidhaniwa kuwa ni paundi milioni kumi na mbili.
Everton,ilitoka sare ya goli 1-1 mwishoni mwa juma lililopita na timu ya Tottenham , wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Sunderland Lamine Kone huku nia ikiwa wazi ya kusalia na mshambuliaji Romelu Lukaku.
Mfanya biashara mkuwa kutoka nchini Irani Farhad Moshiri amenunua hisa asilimia 49.9 % katika timu ya Everton mapema mwaka huu mnamo mwezi wa pili , na kuhitimisha ukame wa muongo mzima wa kusaka uwekezaji mpya.

CHANZO: BBC

Download Music: Young Killer – Mtafutaji

Kutoka pande za Mwanza anakwenda kwa jina la Young Killer na safarii hii katuletea kitu kipya kabisa, ni ngoma iliyo pewa jila Mtafuji ambapo ngoma hiyo imeandaliwa na Producer T-Touch. Humu ndani bhana jamaa kaimba doh! Tusimalize uhondo. 
Bofya hapo chin kuupakua wimbo huo.

Video Mpya: Fid Q Ft. Christian Bella – Roho..

Tizama hapa video mpya kutoka kwa Rapper Nguli kutoka hapa nyumbani na wala sii mwingine bali ni Fid Q akiwa kamshirikisha vyema Christian Bella, Ngoma hiyo ina kwenda kwa jina la Roho. Tizama video hiyo hapo chini.

Wenger: Hatukujiandaa inavyostahili

Arsene Wenger
Arsenal haikuwa na mda wa kuwaanda wachezaji wake baada ya michuano ya Euro2016 na hawakuwa na uzoefu katika mechi walioshindwa na Liverpool kwa mabao 4-3 kulingana na mkufunzi Arsene Wenger.

The Gunners walioongoza 1-0,walifungwa mara tatu katika kipindi cha pili na hivyobasi kuwalazimu kuanza ligi ya Uingereza na kipigo.
Baadhi ya wachezaji waliorudi walikuwa hawako tayari,alisema Wenger ambaye alizomwa na mashabiki katika uwanja wa Emorates.
''Tulilazimika kuadhibiwa.Ni hali ambayo lazima uadhibiwe''

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...