15 August, 2016

Mchezaj Yannick Bolasie asajiliwa rasmi na Club ya Everton

london
Everton imemsajili mchezaji wa kimataifa Yannick Bolasie raia wa Dr Congo anayechezea timu ya Crystal Palace kwa gharama ya paund milioni 25, kwa mkataba wa miaka 5.Bolasie, mwenye umri wa miaka 27, alitumia misimu minne akiwa na timu ya Palace baada ya kujiunga na timu ya Bristol City ya mjini London mwaka 2012.

Amesukuma gozi mara 143 akiwa na timu ya Palacena kufanikiwa kufunga magoli kumi na tatu , na baadaye akabadilika na kuwa kiungo mbadala katika mechi ya mwishoni mwa wiki iliyopita pale timu yake ilipofungwa na West Brom bao moja kwa nunge.
Meneja wa timu ya Palace Alan Pardew alisema baada ya kufungwa bao moja kwa yai tulitambua kuwa moyo na nafsi yake ziko viko mahali kwingine
Bolasie anasema kwamba uamuzi wa kuhamia upande wa Mersey haukuwa wa busara na kuongeza kwamba lakini sasa nimeibukia Everton, kazi haijafanyika bado .Napaswa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kujisikia nimo ndani yake.Niko tayari kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yangu.sio suala la pesa kwa upande wangu ,suala ni kutimiza malengo ya baadaye ya klabu na kule ambako wanatarajia kuifikisha, napenda tu kucheza mpira.
Naye meneja wa timu ya Everton Ronald Koeman anasema kwamba mchezaji huyo Yannick ni mchezaji aliyekuwa anamnyemelea muda mrefu ulio pita kwasababu ni aina ya winga anaye mpenda ,kwanza ana kasi,ana nguvu, na anao uwezo mkubwa wa kucheza katika nafasi mbali mbali hasa mstari wa mbele.

Bolasie ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Everton katika majira haya .
Moja ya majembe hayo yaliyosajiliwa ni pamoja na mlinda mlango Maarten Stekelenburg anatokea timu ya Fulham, Idrissa Gueye kutoka Aston Villa, wakati kiongozi wa timu ya Wales Ashley Williams aliungana na timu hiyo tarehe kumi ya mwezi huu akitokea Swansea kwa ada isiyojulikana, huku ikidhaniwa kuwa ni paundi milioni kumi na mbili.
Everton,ilitoka sare ya goli 1-1 mwishoni mwa juma lililopita na timu ya Tottenham , wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Sunderland Lamine Kone huku nia ikiwa wazi ya kusalia na mshambuliaji Romelu Lukaku.
Mfanya biashara mkuwa kutoka nchini Irani Farhad Moshiri amenunua hisa asilimia 49.9 % katika timu ya Everton mapema mwaka huu mnamo mwezi wa pili , na kuhitimisha ukame wa muongo mzima wa kusaka uwekezaji mpya.

CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...