02 February, 2016

RONALDO APIGA HAT TRICK REAL MADRID IKISHINDA 6-0 LA LIGA

Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kufunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Espanyol kwenye mchezo wa La Liga usiku wa Jumapili Uwanja wa Bernabeu. Mabao mengine ya Real yamefungwa na Karim Benzema, James Rodriguez na Oscar Duarte aliyejifunga.Real Madrid's James Rodriguez celebrates with Luka Modric in a comfortable outing for Zinedine Zidane's sideKarim Benzema rises to give his side the lead with a powerful header at the Santiago Bernabeu on Sunday The Frenchman was delighted with his strike and it set the tone for a one-sided affair at the Bernabeu

HII NDIYO KLABU ILIYOTUMIA MKWANJA MREFU KWENYE USAJILI WA DIRISHA DOGO EPL

Newcastle
Newcastle United imeshindwa kuinasa saini ya Saido Berahino kwenye kipindi cha dirsha dogo la usajili lakini kocha wa timu hiyo Steve McClaren amefanikiwa kuwanasa wachezaji watatu ambao ni Jonjo Shelvey, Andros Townsend na Henri Saivet na kuishuhudia klabu hiyo ikiongoza kwa kutumia kitita kikubwa cha pesa kwenye ligi kuu ya England.
Newcastle imetumia kiasi cha £28.5millioni kwa usajili wa wachezaji hao watatu, wamefanikiwa pia kumnasa Seydou Doumbia kwa mkopo.
Newcastle 1
Newcastle imetumia kiasi cha £70m kwa ajili ya usajili wa msimu wa 2015-16 ikiwa ni kiasi kikubwa cha pesa zaidi ya klabu yeyote ndani ya Premier League.
Kiungo wa kimataifa wa England Jonjo Shelvey amesajiliwa na Newcastle kutoka Swansea City kwa dau la £12million wakati Andros Townsend from yeye amejiunga na Newcastle United pia kwa kiasi cha £12millioni akitokea Tottenham.
Newcastle 2

Wanawake wajawazito wameshauriwa kutosafiri kwenda Brazil kushuhudia mashindano ya Olimpiki mwaka 2016


Wanawake wajawazito wameshauriwa kutosafiri kwenda Brazil kushuhudia mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 kwa sababu ya hatari ya virusi vya Zika.
Serikali ya Brazil imesema kuwa hawashauri wanawake wajawazito kwenda kwenye michezo ya Olimpiki jijini Rio De Jeneiro mwezi Agosti
hatua hii imekuja punde baada ya shirika la afya duniani WHO kutangaza hali ya dharura kutokana na madhara yatokanayo na virusi vya Zika.

Seneta wa Texas Ted Cruz amemshinda Trump mchujo wa Iowa

Trumpeneta wa Texas Ted Cruz ameshinda mchujo wa uchaguzi wa mgombea wa uchaguzi wa Republican katika jimbo la Iowa, Marekani.
Huo ndio mchujo wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa 2016 ambao utafanyika baadaye mwezi Novemba.
Mfanyabiashara Donald Trump alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni kabla ya kura kupigwa lakini sasa dalili zinaonyesha kwamba atakuwa wa pili.
Seneta wa Florida Marco Rubio anaonekana kufanya vyema kuliko ilivyotarajiwa, na huenda akamaliza nambari tatu.
Kura za mchujo wa chama cha Democratic bado zinahesabiwa.
Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya Hillary Clinton na mshoshialisti wa chama cha Democratic Bernie Sanders ni 1% pekee.
Akizungumza baada ya matokeo kujulikana, Marco Rubio amempongeza Bw Cruz na kusema ndiye mgombea ambaye anaweza kuunganisha chama cha Republican ambacho kimegawanyika.CruzWagombea wawili wamejiondoa kinyang’anyironi.
Duru za karibu na mgombea wa Democratic Martin O'Malley, aliyekuwa gavana Maryland, zimeambia BBC kwamba atasitisha kampeni yake, na kufanya ushindani mkali sasa kuwa kati ya wagombea wawili.
Upande wa Republican, gavana wa zamani wa Arkansas Mike Huckabee ameandika kwenye Twitter kwamba atasitisha kampeni yake.

Habari katika magazeti leo February 2,2016


m

01 February, 2016

Muungano wa Afrika AU hautatuma kikosi cha walinda amani hadi pale serikali ya rais Burundi


Msemaji wa Muungano wa Afrika AU, amesema kuwa umoja huo hautatuma majeshi ya kulinda amani nchini humo hadi pale watakapopokea mwaliko kutoka kwa taifa hilo la kanda ya Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ni kinyume na pendekezo la awali la umoja huo ambao uliibua taharuki kuhusu uhalali wake na wajibu wake wa kulinda maisha ya wananchi.
Mjumbe maalum wa umoja huo kanda ya maziwa makuu Ibrahima Fall, anasema kuwa haijawahi kuwa nia ya AU kutuma walinda amani, bila ya idhini ya taifa husika.
Mkutano wa viongozi na marais wa Afrika huko Ethiopia ulishindwa kupitisha mswada uliohitajika ilikuwatuma wanajeshi wapatao 5000 kulinda amani nchini Burundi kufuatia mauaji ya mamia ya wapinzani wa rais Nkurunziza.
Machafuko nchini humo yalitibuka baada ya Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania uchaguzi katika muhula wake wa tatu.
Wapinzani wake walisema Nkurunziza alikuwa anakiuka katiba ya taifa na kisha maandamano yakaanza kukotokea hata jaribio la mapinduzi ambayo ilizimwa na kisha rais huyo akaibuka mshindi katika uchaguzi ambao ulisusiwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa upinzani.
Kulikuwa na pendekezo la kutuma kikosi cha wapiganaji 5,000 wa muungano wa Afrika ilikuokoa maisha ya wapinzani wa rais huyo.
Awali rais Nkurunziza alionya kuwa majeshi yake yangewakabili vikali jeshi hilo ''Vamizi'' akisema kuwa nchi hiyo iko salama na kuwa ni vitongoji vichache tu vya Bujumbura ambavyo ni ngome ya upinzanani.
Kauli ya mwaka jana wa Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu ilisababisha vurugu nchini humo, ambapo mamia ya watu wameuwawa na wengine wengi wakitorokea mataifa jirani.

Marekani kutowa msaada zaidi kwa Ethiopia kukabiliana na ukame

Mkulima nchini Ethiopia katika eneo la Megenta  Afar, Ethiopia, Januari,  2016.
Idara ya misaada ya maendeleo ya Marekani USAID, imetangaza kutowa dola millioni 97 ya msaada wa dharura kwa Ethiopia kusaidia kukabiliana na mzozo unaoendelea wa kibinadam, ulosababishwa na athari za mfumo wa El Nino.
Serikali ya Marekani inasaidia waethopia kukabiliana na athari za El Nino na msaada wetu wa ziada utasidia kujenga juhudi za kushugulikia hali hiyo inayoendelea, alisema mratibu wa USAID Gayle Smith, katika taarifa ilotolewa jana.
Idara ya USAID inaeleza kuwa hali ya jotojoto ilotanda katika bahari ya Pacific, imeathiri kwa kiasi kikubwa mifumo ya hali ya hewa , na  kuharibu uzalishaji wa kilimo, na kufanya maisha kuwa magumu, na kadhalika usalama wa chakula miongoni mwa watu masikini na dhaifu.
USAID inaeleza kuwa msaada huo unajumlisha zaidi ya tani elfu 176 ya chakula ambacho kitasambazwa kwa waethiopia na wakimbizi takriban millioni nne.
Katibu mkuu wa umoja mataifa Bw Ban Ki Moon, alionya jana kuwa Ethiopia inakumbwa na ukame mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30. Alisema, kiwango cha dharura kinachokabiliwa na Ethiopia ni kikubwa mno kwa taifa moja kuweza kukabiliana nayo pekee yake.
Umoja mataifa unaeleza kwamba watu millioni 10 wanahitaji chakula huko Ethiopia, na kuongezea kuwa, idadi hiyo inaweza kuongezeka maradufu katika kipindi cha miezi 9.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...