02 February, 2016

HII NDIYO KLABU ILIYOTUMIA MKWANJA MREFU KWENYE USAJILI WA DIRISHA DOGO EPL

Newcastle
Newcastle United imeshindwa kuinasa saini ya Saido Berahino kwenye kipindi cha dirsha dogo la usajili lakini kocha wa timu hiyo Steve McClaren amefanikiwa kuwanasa wachezaji watatu ambao ni Jonjo Shelvey, Andros Townsend na Henri Saivet na kuishuhudia klabu hiyo ikiongoza kwa kutumia kitita kikubwa cha pesa kwenye ligi kuu ya England.
Newcastle imetumia kiasi cha £28.5millioni kwa usajili wa wachezaji hao watatu, wamefanikiwa pia kumnasa Seydou Doumbia kwa mkopo.
Newcastle 1
Newcastle imetumia kiasi cha £70m kwa ajili ya usajili wa msimu wa 2015-16 ikiwa ni kiasi kikubwa cha pesa zaidi ya klabu yeyote ndani ya Premier League.
Kiungo wa kimataifa wa England Jonjo Shelvey amesajiliwa na Newcastle kutoka Swansea City kwa dau la £12million wakati Andros Townsend from yeye amejiunga na Newcastle United pia kwa kiasi cha £12millioni akitokea Tottenham.
Newcastle 2

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...