Mshambuliaji
Cristiano Ronaldo akikimbia kushangilia baada ya kuifungia mabao mawili
Real Madrid katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Sporting Gijon kwenye mchezo
wa La Liga usiku huu Uwanja wa Bernabeu. Mabao mengine ya Real
yamefungwa na Karim Benzema mawili na Gareth Bale moja, wakati la Gijon
limefungwa na Isma Lopez 18 January, 2016
RONALDO NA BENZEMA KILA MMOJA AFUNGA MAWILI REAL MADRID YASHINDA 5-1 (Video)
Mshambuliaji
Cristiano Ronaldo akikimbia kushangilia baada ya kuifungia mabao mawili
Real Madrid katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Sporting Gijon kwenye mchezo
wa La Liga usiku huu Uwanja wa Bernabeu. Mabao mengine ya Real
yamefungwa na Karim Benzema mawili na Gareth Bale moja, wakati la Gijon
limefungwa na Isma Lopez Mamlaka nchini Marekani zimesema zinajaribu kuwatafuta raia wa Marekani waliopotea mjini Baghdad nchini Iraq.
Watu watatu waliopotea wanahofiwa kutekwa nyara na wanamgambo, chombo cha habari cha al-Arabiya, kimenukuu vyanzo vyake.
''tuna taarifa kuhusu kupotea kwa raia wa Marekani nchini Iraq''. Maafisa wameeleza.
Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini Iraq Scott Bolz amesema wanashirikiana na mamlaka za Iraq kuwatafuta.
Tukio hilo limetokea baada ya muda wa wiki moja paliposhuhudiwa kuzorota kwa hali usalama mjini Baghdad.
Wanamgambo wa Islamic state walikiri kutekeleza mashambulizi kadhaa mjini Baghdad na Dyala wiki iliyopita ambapo zaidi ya watu 50 walipoteza maisha.
Mwandishi wa 'Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe' afariki
Mwandishi maarufu wa tamthilia na kitabu cha ‘Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe’, Edwin Semzaba amefariki jana.
Mbali
na kuwa mwandishi maarufu, Semzaba alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam. Pia, alikuwa mwenyekiti wa Umoja Wa Waandishi wa
Vitabu Tanzania (UWAVITA).
Semzaba
ambaye kitabu chake cha Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe kilimpatia
umaarufu mkubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, aliwahi kueleza kuwa
alianza kuandika kitabu hicho akiwa anasoma kidato cha pili akiwa na
umri wa miaka 16 tu.
Aliimalizia
kazi yake hiyo nzuri baadae ambapo ilikubalika na kuanza kurushwa
kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na baadae kuiweka katika
kitabu kilichokubalika na kutumika kama kitabu cha kiada kwa shule za
sekondari.
17 January, 2016
Rapa Rick Ross amaliza mkataba wake na Def Jam Records, sasa yuko Epic Records.
Ijumaa ya Jan 15 picha ya Rozay akiwa na bosi wa Epic Records aliyewahi kuwa bosi wa Def Jam L.A Reid ilitolewa na kurasa za lebel hio ikiwa na ujumbe “Welcome @rickyrozay to the #EPIC family!”
Rozay alijiunga na Def Jam mwaka 2006 na ametoa album nane mpaka sasa yamwisho ikiwa Black Market iliyoshika namba 6 kwenye bilboard charts.
Rozay atakuwa lebel moja na wasanii kama Future, Diddy, Mariah Carey, Ciara, Travis Scott,na Fifth Harmony.
Wimbo mpya wa Tyga Ft Chris Brown ‘Rumorz’
CHAN 2016:DRC yaichapa Ethiopia
Timu ya DRC imeanza kampeni yake ya
kutaka kushinda kombe la Ubingwa wa Afrika kwa mara ya pili vyema baada
ya kuicharaza Ethiopia 3-0 katika mechi ya ufunguzi wa kundi Ba.
DR
Congo ilioshinda michuano ya CHAN mwaka 2009,ilitawala mechi hiyo
iliochezwa katika mji wa Butare nchini Rwanda,huku Guy Lisadisu
akiwaweka kifua mbele kunako dakika ya 44.Baada ya mapumziko ,Chui hao wa DRC waliendeleza juhudi zao na kunako dakika ya 46 Heritier Luvumbu alifunga kupitia kichwa huku Mechack Elia akiongeza bao la tatu dakika tisa baadaye.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
Mpenzi msomaji wa safu hii ni siku nyingine tunakutana katika kujuzana,kukumbushana, na kuelimishana mila na desturi za makabila mbalimbal...
-
This is a song sang by a very gifted woman Adele, I sang it to show world that everyone appreciate and love to enjoy good music! Asa...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...














