17 January, 2016

CHAN 2016:DRC yaichapa Ethiopia


Timu ya DRC imeanza kampeni yake ya kutaka kushinda kombe la Ubingwa wa Afrika kwa mara ya pili vyema baada ya kuicharaza Ethiopia 3-0 katika mechi ya ufunguzi wa kundi Ba.
DR Congo ilioshinda michuano ya CHAN mwaka 2009,ilitawala mechi hiyo iliochezwa katika mji wa Butare nchini Rwanda,huku Guy Lisadisu akiwaweka kifua mbele kunako dakika ya 44.
Baada ya mapumziko ,Chui hao wa DRC waliendeleza juhudi zao na kunako dakika ya 46 Heritier Luvumbu alifunga kupitia kichwa huku Mechack Elia akiongeza bao la tatu dakika tisa baadaye.Hatua hiyo ina maanisha kwamba timu ya Walia kutoka Ethiopia wanatafuta ushindi wao wa kwanza katika historia ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...