18 January, 2016
Mamlaka nchini Marekani zimesema zinajaribu kuwatafuta raia wa Marekani waliopotea mjini Baghdad nchini Iraq.
Watu watatu waliopotea wanahofiwa kutekwa nyara na wanamgambo, chombo cha habari cha al-Arabiya, kimenukuu vyanzo vyake.
''tuna taarifa kuhusu kupotea kwa raia wa Marekani nchini Iraq''. Maafisa wameeleza.
Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini Iraq Scott Bolz amesema wanashirikiana na mamlaka za Iraq kuwatafuta.
Tukio hilo limetokea baada ya muda wa wiki moja paliposhuhudiwa kuzorota kwa hali usalama mjini Baghdad.
Wanamgambo wa Islamic state walikiri kutekeleza mashambulizi kadhaa mjini Baghdad na Dyala wiki iliyopita ambapo zaidi ya watu 50 walipoteza maisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment