25 May, 2016

Abert Mangwea Mkali wa Free-style aliye ondoka na Kipaji chake.

Hakika hujafa hujaumbika, na Mwanadamu ni uvumbi na atarudi mavumbini, Kifo na mauti havitokwepeka kwa mwanadamu/ama kiumbe chochote chenye Uhai hapa ulimwenguni.

Ikiwa week hii ni week ya kumkumbuka mkali Albert Mangea(a.k.a Mimi), yapo meengi yamepita tangu kuondoka kwake, na hasa katika game hili la Muziki wa Bongo Flava, wapo wasanii wapya pia katika game hili na muziki huu umekua na kukua kweli kweli na natamani mkali huyu ange kuwako katika enzi hizi, sipati picha.

Historia yake Kwa ufupi..

Alizaliwa na jina la Albert Keneth Mangwair mnamo tar. 16 Novemba, 1982, Mbeya, Tanzania. Kiasili, ni mtu wa Ruvuma, yaani, ni Mngoni. Lakini alizaliw mjini Mbeya na akiwa na umri wa miaka 5, familia yake ilihamia mjini Morogoro kikazi na hatimaye kuanza masomo ya msingi hukohuko mjini Morogoro hadi darasa la 5 na kupata uhamisho wa kwenda Dodoma ambapo aliweza kujiunga na shule ya msingi ya Mlimwa. Kisha baadaye shule ya Sekondari ya Mazengo na Chuo cha Ufundi cha Mazengo.

Katika ngazi ya familia, yeye ni mtoto wa mwisho (kwa baba akiwa mtoto wa 10) - na (kwa mama akiwa mtoto wa 6). Albert alifariki dunia mnamo tar. 28 Mei katika mwaka wa 2013 kwa hicho kinachoaminiwa kwamba alizidisha kipimo cha dawa za kulevya huko nchini Afrika Kusini. Ngwair aliacha mtoto mmoja.

Kazi na Muziki..

Ngwair alikuwa akiishi jijini Dar es Salaam, Tanzania ambako alikokutana na mtayarishaji mahiri wa mziki P. Funk Majani na kuanza kufanya naye kazi. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2003 ambapo alitoa kibao cha kwanza kiitwacho 'Ghetto Langu,' wimbo uliompatia umaarufu mkubwa sana.

Mangwair pia aliwahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. Mwaka wa 2007 akatokea kwa wimbo wa kimya kimya akiwa na wana chemba. Katika Kimya Kimya anapagawisha.Zipo nyimbo nyingi ambazo Mangwea alitisha nazo kama Vile Gheto langu, Mikasi, CNN, she got gwan, Dakika moja, Mungu Nisamehe, na pia alipata colabo zilizo hit kama ile ya May Baby yake Quick Raka, na nyingine kibao.

Kifo na mauti...

Albert Mangwair alifariki tarehe 28/5/2013 akiwa huko Afrika ya Kusini. Taarifa zinasema alifariki baada ya kutumia madawa ya kulevya lakini kuna utata kuhusu kilichosababisha kifo cha marehemu, licha ya baadhi ya mitandao mbali mbali kuandika chanzo cha kifo cha mkali huyu ila baadae iligundulika kwamba alilewa kupindukia ilhali hakua amekula.(Rest in peace Mangwea).

 Pengo la mangwea katika Bongo Flava/Jamii...

Hakika itachukua Muda mrefu kwa pengo lake kuzibika ama hata Pengo lake kutozibika daima maana kipaji chake na mtazamo wake ulikuwa ni wa hali ya juu mno. Mashairi yake yaliburudisha, Kuelimisha jamii. Mchango wako utakumbukwa na wengi wakubwa ama wadogo, Muziki wa bongo Flava utakukumbuka kwa mchango wako mkubwa uliokua ukiutoa ili mradi tuu uone muziki huo ukisonga mbele na kukua.

Tizama Moja kati ya Video ambayo mimi naipenda kutoka kwa Mkali huyu wa free style( Kimya kimya)


Utakumbukwa na wana kibao, washkaji zako wakina J-Moe, Wana Chemba, T.I.D, Bongo Records na wengine kibao ambao walikuepo kipindi ukiwa china na hata kipindi ukiwa nazo(Marafiki wa dam dam). Mashabiki zako Tutakukumbuka kwa ngoma zako za kinyamwezi na Flow zenye mautam na zaidi ya yote tutazikumbuka zile shows zako.

Naamini ngoma zako zikipigwa club yeyote bado mzuka utakua ule ule daima.

 PUMZIKA KWA AMAN MANGWEA, MBELE YAKO NYUMA YAKO.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...