06 October, 2016

Audio Mpya: Jux ft Vanessa--JUU

Umefikia muda wa kuikata kiu yako uliyoitunza kwa muda mrefu. Wapendanao Vanessa Mdee na Jux wameachia bonge moja la kolabo linalokwenda kwa jina la "Juu" ambalo limeachiwa kwa mara ya kwanza kabisa kwenye Mkito. Ngoma hii imetengenezwa na Lufa- Switch Records.

Huu umekuwa mwaka mzuri kwa wawili hawa. Wamepiga tour za kutosha nchini kwenye Fiesta huku wimbo wa "Wivu" wa Jux ukiendelea kusumbua kwenye chati mbalimbali za muziki. Vanessa anatuwakilisha kwenye msimu mpya wa Coke Studio Africa unaoanza jumamosi hii huku pia akiwa mmojawapo wa wasanii wa nyumbani wanaogombania tuzo za MTV Base MAMAs kwenye kipengele cha Msanii bora wa kike. Atakinukisha tena wikiendi hii mjini Mombasa akiwa na wakali kama Wizkid na Chris Brown.
KUUPATA WIMBO HUO BOFYA DOWNLOAD HAPO CHINI.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...