08 October, 2016

Ureno yaichapa Andorra 6-0, Ronaldo aweka Rekodi mpya

ronaldo-42Cristiano Ronaldo amefunga magoli manne wakati Ureno wakitoa kichapo cha magoli 6-0 dhidi ya Andorra kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Ronaldo alifunga magoli mawili moja kwa kichwa jingine kwa mguu ndani ya dakika nne za kipindi cha kwanza na kuwaweka mbele mabingwa wa taji la Euro 2016.

Joao Cancelo aliongeza bao la tatu kisha Ronaldo akafunga goli la tatu kukamilisha hat-trick yake katika mchezo huo.

Ronaldo alirejea kambani kwa mara nyingine kufunga goli lake la nne katika mchezo huo huku likiwa ni goli la tano kwa Ureno kabla ya Andre Silva kuhitimisha party ya magoli dhidi ya Andorra ambao walipoteza wachezaji wao wawili kutokana na kuoneshwa kadi nyekundu.

Ureno kwa sasa wapo nafasi ya tatu katika Kundi B wakiwa wamepoteza mchezo dhidi ya vinara wa kundi hilo Switzerland ambao wameifunga Hungury 3-2 kwenye mchezo wao wa Ijumaa.

Hat-trick hiyo inamfanya Ronaldo aweke rekodi ya kufikisha jumla ya hat-trick 42 katika maisha yake yote ya soka.

Ronaldo alipata majeraha kwenye mchezo wa fainali ya Euro 2016, mchezo dhidi ya Andorra ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza wa kimataifa tangu fainali ya Euro ambapo Ureno ilishinda 1-0 dhidi ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...