Mwanariadha mlemavu kutoka Kenya
Samwel Mushai Kimani ameshindia Kenya dhahabu nyingine baada ya kuibuka
mshindi wa mbio za wanaume mita 1,500 kitengo T11 Paralimpiki.
Kimani aliandikisha muda wa 4:03.25, muda bora zaidi msimu huu.Mbrazil Odair Santos alimaliza wa pili.
Mbio hizo hata hivyo hazikuwa za kasi kama za kitengo T13 ambapo wanariadha wanne waliomaliza wa kwanza waliandikisha muda bora kushinda wa mshindi wa mbio za Olimpiki mita 1,500.
Katika mbio za kitengo T13, raia wa Algeria Abdellatif Baka alishinda na kuandikisha rekodi ya dunia ya 3:48.29. Mshindi wa dhahabu Olimpiki Matthew Centrowitz alitumia muda wa 3:50.00.
Kimani alikuwa ameishindia Kenya dhahabu ya kwanza katika michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Rio 2016 kwa ushindi katika mbio za mita 5,000 kitengo T11 (wanariadha wasioona wakisaidiwa na waelekezi).
Odair Santos alishinda fedha katika mbio hizo naye Erick Sang wa Kenya akatwaa shaba.
Kenya ilishinda dhahabu mbili Paralimpiki za London, na kubeba medali sita kwa jumla.
No comments:
Post a Comment