14 September, 2016

Ligi ya Mabingwa: Barcelona 7-0 Celtic

Celtic hawakuweza kumdhibiti Messi
Celtic walipokezwa kichapo kibaya zaidi katika mashindano ya Ulaya Jumanne usiku baada ya kuchapwa mabao 7-0 na Barcelona uwanjani Camp Nou.
Mshambuliaji Lionel Messi, raia wa Argentina, alifunga 'hat-trick' yake ya sita katika mechi hiyo ya kundi C.
Alianza kwa kufunga bao la mapema

Mchezaji wa Celtic Moussa Dembele alishindwa kufunga penalti kabla ya Messi kufunga la pili.
Kipindi cha pili, Neymar alifunga kupitia frikiki, Andres Iniesta akafunga la nne, Messi akaongeza la tano naye Suarez akakamilisha ushindi kwa mabao ya sita na saba.Neymar baada ya kufunga bao la tatu Camp NouKatika misimu miwili ambayo wamekuwa pamoja Nou Camp, Messi, Neymar na Luis Suarez wamefunga mabao 253 na kusaidia ufungaji wa mabao 120.Andres Iniesta alifunga baada ya kuingia kama nguvu mpya

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...