12 September, 2016

SHILOLE: Jina langu ni Fursa ya mafanikio.

 
Mwanamuziki na Muigizaji Zuenna Muhamed maarufu kama Shilole "SHISHI BABY" amesema Usanii ni mlango wakupitia ili kufuata mafanikio yalipo, huku akiahidi kuifanyia kazi kila nafasi itakayo katiza mbele yake. Akizungumza hivi karibuni, Shilole alisema ukiwa msanii unafahamiana na watu wengi wanao fanya mambo mbali mbali, hivyo ni nafasi yakufahamu mambo mengi pia.

 Shilole alisema tangu muziki hajawahi kukatishwa tamaa wala kufikiria kufanya hivyo licha yakua na mashabiki wa aina mbali mbali wanao kubali kazi zake. Alisema 
" Watu wengi wanatafuta nafasi yakufahamiana na watu wengi ili wapanue uwigo wa uelewa kati yaon na kufanikisha ndoto zao, sasa kwa nini mimi nimepata nafasi hiyo bado mimi nishangae, naifanyia kazi kila Fursa nitakayoiona mbele yangu"
Shilole aliwataka wasanii wakike na wakiume kuwekeza kipindi ambacho wana nguvu ili iwe msaada Baadae. 
"Wasanii hatuna kiinua mgongozaidi yakukikuza kile kidogo tunacho pata, hakuna njia nyingine zaidi ya Biashara, wasichana tupunguze mashindano ya mavazi tandae kiinua mgongo, Vivyo hivyo wavulana wapunguze Bata wajiandalie kiinua mgongo"

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...