13 August, 2016

Sababu kwanini Paul Pogba amefungiwa kucheza vs Bournemouth

Kiungo mpya wa Manchester United Paul Pogba amesimamishwa kuitumikia timu yake kwa mchezo wa kwanza wa Premier League,  chama cha soka cha England kimethibitisha
Pogba, 23, alirejea Old Trafford kutoka Juventus kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya £89.3 million, miaka 4 baada ya kuhamia klabu ya Turin kwa ada ya £800,000 kufuatia kukosa muda wa kucheza na mgogoro wa mkataba mpya. 
Hata hivyo Pogba itambidi asubiri mpaka wiki ijayo kucheza mchezo wake wa kwanza na klabu yake mpya kwa sababu amefungiwa kucheza mchezo wa Jumapili dhidi ya Bournemouth.

Kiungo huyo wa Ufaransa amesimamishwa kwa kosa la kupata kadi mbili za njano katika msimu uliopita wa mashindano ya Coppa Italia, na adhabu yake imehamia katika michezo inayosimamiwa na Chama cha soka cha England

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...