07 August, 2016

Mwanasayansi anyongwa kwa kosa la usaliti huko Iran

Mwanasayansi kutoka Iran Shahram Amiri ameuawa
Iran imethibitisha kwamba imemuuwa mwanasayansi wa nyuklia, ambaye alituhumiwa kwamba aliipa Marekani habari muhimu kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran.

Shahram Amiri alitoweka mwaka wa 2009 alipokwenda kuhiji katika mji mtukufu wa Mecca .
Alipojitokeza mwaka uliofuatia alikuwa nchini Marekani , akisema kuwa alitekwa nyara na CIA.
Kupitia kwa mitandao ya kijamii alidai kuwa alikuwa ametekwa na kuwa aalikuwa akijificha kutoka kwa majasusi wa Marekani.
Lakini alidai kwamba aliweza kutoroka, na alikaribishwa kama shujaa aliporudi Iran.

Video tatu za Shahram Amiri

Lakini baadaye, Bwana Amiri alifikishwa mahakamani.
Marekani imesema bwana Amiri alikwenda Marekani mwenyewe, na kwamba aliwapatia habari muhimu.
Habari za kuuawa kwake ziliibuka jumamosi mamake mzazi aliposema kuwa alipokea mwili wake uliokuwa na alama za kunyongwa shingoni.

Msemaji wa mahakama aliwaambia waandishi wa habari kuwa ''Shahram Amiri alikuwa amewapa maadui wa Iran habari nyeti kuhusiana na mpango wake wa kinyuklia.''
Gholamhossein Mohseni Ejei alinukuliwa akisema.

Awali Amiri alipokewa kwa shangwe na taadhima aliporejea nyumbani.
Iran imekuwa ikitafuta maarifa ya kuunda silaha za kinyuklia japo imekuwa ikipinga kufanya hivyo na badala yake ikisema kuwa inatafuta nguvu mbadala za umeme.

ata hivyo majuzi ilikubaliana na mataifa yenye nguvu zaidi duniani kusitisha mpango huo wa kisiri na badala yake ipokee msaada kutoka kwa mataifa hayo yenye nguvu za kinyuklia.

loading...

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...