27 August, 2016

Music: Emanuel Austin na Rajson Melody – Mapenzi Digitali

Emanuel Austin ni mwalimu wa Dance huko nchini Uingereza,  amekua akifanya kazi na wasanii kadhaa wa hapa nyumbani pia kama vile Ben Paul na wasanii wengine. Na hii ni ngoma yake nyingine alomshirikisha Rajson Melody, wimbo unakwenda kwa jina la ‘Mapenzi Digitali.’ Mkono wa Producer Bako Rapper. 

Bofya DOWNLOAD hapo chini kuupakua wimbo huo.

VideoMPYA: Dogo Janja- Kidebe

Baada ya kufanya poa katika ngoma yake iliyopewa jina la My Life, Mkali kutoka Tip-Top conection, Janjaro safari hii katuletea video yake Mpya inayokwenda kwa jina la Kidebe, Video hii imeongozwa na Director Mkali Director Hanscana. Enjoy Kidebe.  
Bofya DOWNLOAD hapa chini Kupakua Audio ya Kidebe.

Tizama hapa Video mpya ya Msanii Mo Music- Ado Ado

Mwanamuziki anaye fanya poa katika game la Muziki wa bongo Flava Mo Music, anatukaribisha kuitizama video yake mpya Ado Ado. Tizama video hiyo hapo chini kisha washirikishe wana kitaa kwa kadiri uwezavyo. Enjoy Ado Ado.  
Pia unaweza Kuupakua wimbo huo hapa hapa kwa Kubonyeza DOWNLOAD hapo chini.

26 August, 2016

New Music: Sam Misago na Quick Rocka – Vyura na Madanga

Kazi mpya ya mtangazaji wa EATV na rapper Sam Misago akimshirikisha Quick Rocka. Inaitwa Vyura na Madanga na imetayarishwa na Luffa kwenye studio za Switch Records. Bofya DOWNLOAD hapo chini kuupakua wimbo huo.

Droo Europa League: Man Utd kukutana na Robin van Persie

Robin Van Persie
Manchester United watakutana na klabu anayochezea nyota wao wa zamani Robin Van Persie- Fenerbahce- pamoja na Feyenoord na Zorya Luhansk hatua ya makundi Europa League.
Klabu ya KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Ally Samatta imewekwa kundi F na Athletic Bilbao ya Uhispania, Rapid Vienna ya Austria na Unione Sportiva Sassuolo Calcio kwa ufupi Sassuolo ya Italia.
Southampton, klabu nyingine ya Ligi ya England inayocheza michuano hiyo, imepangwa kucheza dhidi ya Inter Milan, Sparta Prague na Hapoel Beer Sheva.
Dundalk ya Ireland nayo imepangwa na h Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar na Maccabi Tel-Aviv baada ya droo kufanywa Monaco.Zlatan Ibrahimovic na Robin van Persie

Meneja wa United Jose Mourinho amesema hawafahamu vyema wapinzani wao Zorya, kutoka Ukraine, lakini amefurahia kuwekwa kundi moja na Fenerbahce na Feyenoord.
"Sote twafahamu kwamba shindano hili si kama Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya lakini kuwa na Manchester United ikikutana na klabu zenye historia ndefu kama vile Fenerbahce na Feyenoord ni jambo zuri kwetu," amesema.

Droo kamili:

Kundi A: Man Utd, Fenerbahce, Feyenoord, Zorya Luhansk
Kundi B: Olympiacos, Apoel Nicosia, Young Boys, Astana
Kundi C: Anderlecht, St Etienne, Mainz, Qabala
Kundi D: Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar, Maccabi Tel-Aviv, Dundalk
Kundi E: Plzen, Roma, Austria Vienna, FC Astra Giurgiu
Kundi F: Athletic Bilbao, Genk, Rapid Vienna, Sassuolo
Kundi G: Ajax, Standard Liege, Celta Vigo, Panathinaikos
Kundi H: Shakhtar Donetsk, Braga, Gent, Konyaspor
Kundi I: Schalke 04, FC Red Bull Salzburg, Krasnodar, Nice
Kundi J: Fiorentina, PAOK Salonika, Liberec, Qarabag
Kundi K: Inter Milan, Sparta Prague, Southampton, Hapoel Beer Sheva
Kundi L: Villarreal, Steaua Bucharest, FC Zurich, Osmanlispor

CHANZO: BBC

Mr. Nice apata shavu la kupiga show 47, ataja wasanii wakubwa waliomuomba kolabo

nic  Mwanamuziki mkongwe katika Burudani ya muziki na mwanzilisha wa ‘Takeu style’, Lukas Mkenda almaarufu kama Mr. Nice, amepata shavu kutoka katika kampuni moja ya Nigeria ambayo imempatia mkali huyo shows 47 ambazo atazifanya katika County mbali mbali huko nchini Kenya ambapo ndipo alipo kwa sasa akiendesha shughuli zake za Muziki. 
“Niko huku Kenya,kuna kampuni ya Nigeria imenipa dili la kufanya tour kwenye county zote za Kenya, ziko 47″ Mr. Nice aliiambia Radion one.

Pia Mr.Nice amesema ana project mpya na Jaguar na Wyre ambazo zitatoke hivi karibuni,
“Pia nina project na wasanii wengine wa Kenya ambao wameniomba nifanye nao kazi,tuko na project na Jaguar na nyingine na Wyre kwa hiyo soon mambo yatakuwa mazuri”
Kila la Kheri Bro!

Wizkid kuungana na Davido Sony Music Worldwide

Mwanamuziki maarufu Nigeria na Africa kwa ujumla Wizkid yuko mbioni kutangazwa msanii mpya wa Sony Music Worldwide, kwa mujibu wa kituo cha runinga cha Soundcity.Kituo hicho kimeripoti kuwa muimbaji huyo ataungana na Davido kwenye roaster ya label hiyo kubwa.
“Dili la Wizkid na Sony limekamilika. Habari itatoka hivi karibuni. Meneja wake Sunday Are ametuelezea kuwa hili litazungumzwa hivi karibuni,” kilisema chanzo.
Umaarufu wa Wizkid umeongezeka maradafu mwaka huu baada ya kushirikishwa na Drake kwenye wimbo One Dance ulioshika namba moja kwenye chati za Billboard Hot 100.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...