
Askofu mkuu wa Canterbury Justin
Welby amemaliza ziara yake nchini Burundi na kufanikiwa kuwa na
mazungumzo na Rais wa Taifa hilo Pierre Nkurunziza.
Mzungumzo hayo
yameangazia umhimu wa kuwepo mazungumzo ya pamoja ili kuepusha mauaji
yanayoendelea kufuatia vurugu zilizozuka kutokana na uamuazi wa Rais wa
taifa hilo kuwania mhula mwingine wa Uongozi.
Mamia ya watu wameuawa kutokana na vurugu hizo huku maelfu wakilazimika kuikimbia nchi yao na kukimbilia nchi jirani.
Rais
Pierre Nkurunziza Katika mazungumzo hayo na kiongozi huyu wa
Kiroho,muda mwingi alionekana ni mwenye furaha na tabasamu mbele ya
ambapo undani wa mazungumzo hayo ilikuwa ni kuhimiza ushiriki wa pande
zote ili kuhakikisha kuwa amani ya kweli inafikiwa nchini humo.
Askofu Just Welby amesema kuwa suala la maridhiano nchini Burundi linahitaji watu kujitoa muhanga.
Hata hivyo amesisitiza hatua za msingi za kuzingatiwa ili kuweza kufikiwa kwa amani ya kweli nchini Burundi.
Taifa
la Burundi lililopata Uhuru wake 1962 na kupitia katika vipindi
mbalimbali vya machafuko limejikuta katika upotevu wa hali ya amani
katika kipindi kingine kufuatia uamuzi wa Rais wa taifa hilo Pierre
Nkurunziza kuamua kuwania muhula mwingine hatua inayopingwa na upinzani
nchini humo.