Mhandisi John William Kijazi ameteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi nchini
Kabla
ya kuteuliwa leo Mhandisi Kijazi alikuwa anahudumu kama balozi wa
Tanzania nchini India ambapo majuzi tu alitoa mchango mkubwa katika
kuhakikisha wanafunzi raia wa Tanzania wanapata usalama kufuatia
shambulizi dhidi ya mmoja wao.Katika taarifa fupi kutoka kwa ikulu ya rais John Pombe Magufuli Balozi huyo anaanza kazi mara moja.
Mhandisi Kijazi anachukua nafasi iliyowachwa wazi baada ya kuondolewa Balozi Ombeni Sefue.
Haijulikani kwanini balozi Sefue ameondolewa katika wadhfa huo ila taarifa hiyo ya ikulu iliyotiwa sahihi na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa inasema kuwa Sefue atapewa majukumu mengine.
No comments:
Post a Comment