07 March, 2016

Simba yaongoza ligi kuu Tanzania bara ni baada ya kuichapa Mbeya City bao 2-0

Wekundu wa Msimbazi Simba Sport Klabu wamechukua usukani wa ligi kuu Tanzania bara baada ya ushindi dhidi ya Mbeya City. Wekundu hao wa msimbazi walipa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao Mbeya City kwa mabao yaliyofungwa na Daniel Lyanga na Ibrahim Ajib. Simba wakiwa kileleni kwa alama 48 wakiwa wamecheza 21 wanafatiwa na wapinzani wao wa jadi Yanga walioko nafasi ya pili wakiwa na alama 47 kwa michezo 20 huku Azam akiwa katika nafasi ya tatu kwa alama 47 pia wakitofautiana na yanga kwa idada ya magoli. Ligi hiyo itaendelea tena hapo Jumanne kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo Yanga, kushuka dimbani kwenye dimba la Taifa kukipiga na African Sports ya Tanga.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...