21 July, 2015

MAN UNITED WAANDAA MZIGO WA €100M KUSAJILI MTAMBO HUU WA BAYERN MUNICH

1172701195-mueller-gaal-1Wef
Kwa muiibu wa chombo cha habari cha Ujerumani cha Sport1, Manchester United wanajiandaa kutuma ofa mpya kumsajili nyota wa Bayern, Thomas Muller.
Awali Man United waliweka mezani ofa ya Euro milioni 82 kuinasa saini ya mshindi huyo wa kombe la Dunia 2014, lakini Miamba ya Bavarian ilikataa.
Wakiwa tayari wamemsajili Gwiji wa Bayern, 
Bastian Schweinsteiger,  Louis van Gaal anajiamini kwamba anaweza kumsajili Muller.
Sport1 wanadai kwamba United wapo tayari kulipa Euro milioni 100 sawa na paundi milioni 69 kumsajili Muller.
Dau hilo limeandaliwa na bosi mwenyewe Ed Woodward.
Kama United watamsajili kwa dau hilo, utakuwa usajili ghali zaidi kuwahi kufanyika na klabu hiyo wakivunja rekodi ya kumnasa Angel Di Maria kwa paundi milioni 59.7 majira ya kiangazi mwaka jana.
Hata hivyo, mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge 
amewaondoa hofu mashabiki kwamba hakuna mchezaji atakayeuzwa kwasasa.

Video: Emanuel Austin Ft. Ben Pol – 'Ruka Juu'

Video kali ya wimbo wa msanii na mwalimu wa dance anayeishi nchini Ujerumani, Emanuel Austin aliomshirikisha Ben Pol. Video iliongozwa na mmoja wa waongozaji maarufu nchini Ujerumani.

Diamond Platnumz anawania vipengele saba kwenye tuzo za AFRIMMA 2015.

dp5
Baada ya kushinda tuzo moja kwenye Mtv Afrika Music Awards, msanii Diamond Platnumz ametajwa kuwania vipengele saba kwenye tuzo za AFRIMMA 2015, Hivi ndivyo vipengele alivyotajwa na alichowaandikia mashabiki wake.
Eeeh Mwenyez Mungu Baba nakushkuru sana kwa kuendelea kubariki Kazi yangu… Siku zote nitaendelea kuwa Mwema na kuhakikisha nafanya kazi kwa bidii… 6 NOMINATIONS ON AFRIMA AWARDS…
1. Best Artist Of the Year
2. Best Dance Video (Nana)
3. Best Video (Ntampata Wapi)
4. Best East Artist of the Year
5. Best Collaboration (Nana)
6. Song of the Year (Ntampata Wapi)
7. Best Inspiration Song: Alive by Bracket ft Diamond platnunz & Tiwasavage…
Thanks alot @Afrimma for recognizing my Work.. i wish you Guys can understand how these Nominations means to me…. thanks alot to all Media Houses for keep supporting my Music without forgetting My Die Hard Fans #TeamWasafi na Wote wapenda Muziki wa Bongoflavour!!! ”

20 July, 2015

Video: Baada ya ushindi wa Tuzo za MTV, Davido athibitisha ujio wa collabo mpya na Diamond mwezi ujao

Baada ya wote wawili kuibuka washindi kwenye tuzo za MTV MAMA 2015 zilizotolewa Jumamosi iliyopita Durban, Afrika Kusini, Davido na Diamond wameweka wazi ujio wa collabo yao mpya.

Wakiwa na furaha huku wakiwa wamebeba tuzo zao mikononi mara baada ya tukio la utolewaji tuzo hizo kuisha, staa wa Nigeria Davido akiwa na Diamond ametoa ahadi ya collabo yao mpya.

Katika kipande cha video (hapo chini) Davido ametamka kwa kinywa chake:

“New F*ckin Diamond and Davido we gonna dropin next month, we do this f*ckn East Africa West Africa biggest artist we do this…we are uniting…” Wakati Davido akiyaongea hayo, Diamond alikua akiitikia “I’m telling you”.

Diamond aliibuka mshindi wa tuzo ya ‘Best Live Act’ na Davido naye aliibuka mshindi wa tuzo kubwa ya Best male ambayo pia alishinda mwaka jana.

Irene Uwoya Naye ajitosa kwenye Siasa......Achukua fomu ya Ubunge viti maalum Tabora

Msanii  wa  Bongo  movie, Irene  amechukua  fomu  ya  kugombea  ubunge  wa Viti  Maalum  kwa  tiketi  ya  CCM  huko  Tabora.
  Hizi  ni  picha  alizotutumia  wakati  akikabidhiwa  fomu  hiyo.


HAWA NDO WAAMUZI WALIOTEULIWA KUCHEZESHA EPL MSIMU WA 2015-16

article-2610413-1D34710000000578-78_634x455
Kuna jamaa mmoja kanipigia simu ila mtandao huku kwetu Monduli juu unasumbua sana!! lakini kwa mbaali nilimskia akisema, “….watajutia
maamuzi yao…” lakini simu yake ilikuwa inakata kata sana. Lengo langu lilikuwa kumuuliza…. vipi Waamuzi wa michuano ya Kagame
wanaeleweka???
Kutokana na Waamuzi kuwa muhimu sana katika tathnia ya soka, leo nimeona nitazame Waamuzi wanaotarajiwa kuchezesha takribani mechi 380 za ligi kuu ya Uingereza ambayo siku chache zijazo inaanza kutimua vumbi katika viunga tofauti vya miji mbalimbali ya pale England.
Ebwana kabla ya kukutajia Waamuzi wanaotarajiwa kuchezesha mechi mbalimbali pale Epl, ni vyema ukafahamu mchakato mzma wa kuwapata
Waamuzi hawa, kwa kuanzia ni kwamba kuna chombo kinaitwa “Professional Game Match Officials Board” chini ya Mwamuzi wa zamani Mike Relay.
Chombo hiki kiliundwa na chama cha waamuzi wa soka pale England, chini ya Relay. Pia kuna kamati zingine ambazo hutekeleza majukumu ya uteuzi wa Waamuzi kwa kuzingatia uzoefu na umakini katika mechi za ligi.
 Pia
chombo hiki kina kazi ya kuajiri Waamuzi wapya na kuwapandisha daraja Waamuzi wanaoonekana kufanya vyema ngazi za chini,
Lakini kama unavyofahamu majina ya Waamuzi 15-20 ambao watachezesha mechi za kila wiki hutajwa mwanzo wa msimu, lakini suala la mechi gani nani atachezesha mara nyingi hupangwa siku chache kabla ya mechi husika ili kuepusha njama za upangaji matokeo, hapa chini nimekuwekea Waamuzi wote watakaochezesha mechi za Epl msimu wa 2015-16….
Waamuzi  na umri wao
1 Martin Atkinson {43}
2 Mark Clattenburg {39}
3 Mike Dean {46}
4 Phil Dowd {51}
5 Roger East {49}
6 Chris Foy {52}
7 Kevin Friend {43}
8 Mike Jones {46}
9 Robert Madley {29}
10 Andre Marriner {44}
11 Lee Mason {43}
12 Jonathan Moss {44}
13 Michael Oliver {29}
14 Craig Pawson {35}
15 Lee Probert {42}
16 Neil Swarbrick {49}
17 Anthony Taylor {36}

Collabo ya Donald na Diamond Platnumz iko hewani, wimbo unaitwa “Wangu” na hii ndio Video yake!

.
Baada ya kusuburi kwa muda mrefu ule wimbo wa Donald wa South Africa na Diamond Platnumz hatimaye umesogezewa kwetu rasmi leo Julai 20 2015.
Wimbo unaitwa Wangu na hii hapa chini ndio official video ya wimbo wao. Bonyeza Play kuitazama.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...