Kwa muiibu wa chombo cha habari cha Ujerumani cha Sport1, Manchester United wanajiandaa kutuma ofa mpya kumsajili nyota wa Bayern, Thomas Muller.
Awali Man United waliweka
mezani ofa ya Euro milioni 82 kuinasa saini ya mshindi huyo wa kombe la
Dunia 2014, lakini Miamba ya Bavarian ilikataa.
Wakiwa tayari wamemsajili Gwiji wa Bayern,
Bastian Schweinsteiger, Louis van Gaal anajiamini kwamba anaweza kumsajili Muller.
Sport1 wanadai kwamba United wapo tayari kulipa Euro milioni 100 sawa na paundi milioni 69 kumsajili Muller.
Dau hilo limeandaliwa na bosi mwenyewe Ed Woodward.
Kama United watamsajili kwa dau
hilo, utakuwa usajili ghali zaidi kuwahi kufanyika na klabu hiyo
wakivunja rekodi ya kumnasa Angel Di Maria kwa paundi milioni 59.7
majira ya kiangazi mwaka jana.
Hata hivyo, mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge
amewaondoa hofu mashabiki kwamba hakuna mchezaji atakayeuzwa kwasasa.
No comments:
Post a Comment