20 July, 2015
HAWA NDO WAAMUZI WALIOTEULIWA KUCHEZESHA EPL MSIMU WA 2015-16
Kuna jamaa mmoja kanipigia simu ila mtandao huku kwetu Monduli juu unasumbua sana!! lakini kwa mbaali nilimskia akisema, “….watajutia
maamuzi yao…” lakini simu yake ilikuwa inakata kata sana. Lengo langu lilikuwa kumuuliza…. vipi Waamuzi wa michuano ya Kagame
wanaeleweka???
Kutokana na Waamuzi kuwa muhimu sana katika tathnia ya soka, leo nimeona nitazame Waamuzi wanaotarajiwa kuchezesha takribani mechi 380 za ligi kuu ya Uingereza ambayo siku chache zijazo inaanza kutimua vumbi katika viunga tofauti vya miji mbalimbali ya pale England.
Ebwana kabla ya kukutajia Waamuzi wanaotarajiwa kuchezesha mechi mbalimbali pale Epl, ni vyema ukafahamu mchakato mzma wa kuwapata
Waamuzi hawa, kwa kuanzia ni kwamba kuna chombo kinaitwa “Professional Game Match Officials Board” chini ya Mwamuzi wa zamani Mike Relay.
Chombo hiki kiliundwa na chama cha waamuzi wa soka pale England, chini ya Relay. Pia kuna kamati zingine ambazo hutekeleza majukumu ya uteuzi wa Waamuzi kwa kuzingatia uzoefu na umakini katika mechi za ligi.
Pia
chombo hiki kina kazi ya kuajiri Waamuzi wapya na kuwapandisha daraja Waamuzi wanaoonekana kufanya vyema ngazi za chini,
Lakini kama unavyofahamu majina ya Waamuzi 15-20 ambao watachezesha mechi za kila wiki hutajwa mwanzo wa msimu, lakini suala la mechi gani nani atachezesha mara nyingi hupangwa siku chache kabla ya mechi husika ili kuepusha njama za upangaji matokeo, hapa chini nimekuwekea Waamuzi wote watakaochezesha mechi za Epl msimu wa 2015-16….
Waamuzi na umri wao
1 Martin Atkinson {43}
2 Mark Clattenburg {39}
3 Mike Dean {46}
4 Phil Dowd {51}
5 Roger East {49}
6 Chris Foy {52}
7 Kevin Friend {43}
8 Mike Jones {46}
9 Robert Madley {29}
10 Andre Marriner {44}
11 Lee Mason {43}
12 Jonathan Moss {44}
13 Michael Oliver {29}
14 Craig Pawson {35}
15 Lee Probert {42}
16 Neil Swarbrick {49}
17 Anthony Taylor {36}
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment