Baada ya klabu ya Chelsea kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England..sasa wameanza mikakati ya kukiboresha kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu. Kipa wao Petr Cech
baada ya kuitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2004 uongozi wa timu yake
umempa uhuru wa
kufanya mazungumzo na timu nyingine zinazowania saini yake.
kufanya mazungumzo na timu nyingine zinazowania saini yake.
Wakala ya kipa huyo Viktor Kolar, amethibitisha kuruhusiwa kufanya mazunguzo kwa mteja wake na timu yoyote inayomuhitaji .
Hivi karibuni Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
alisema anamuhitaji kipa huyo kuendelea kuitumika klabu hiyo kw amsimu
unaokuja na kusisitiza bila uwepo wake klabu hiyo isingeweza kutwaa taji
hilo.
Hata hivyo sababu kubwa inayopelekea kipa huyo kuhama ni kucheza Chelsea akiwa chagua la pili huku namba moja akiwa Thibaut Courtois na bosi wake Mourhinho amemtaka hata kama atahama asizichezee klabu za ligi kuu ya England.
No comments:
Post a Comment