02 September, 2016

Brazil, Argentina zashinda kufuzu kombe la dunia 2018

Mshambuliaji wa Brazil Neymer Jr
Michezo ya kuwania kuzufu kwa fainali za kombe la dunia zitazofanyika nchini Urusi mwaka 2018, kwa ukanda wa Amerika kusini, zimechezwa usiku wa kuamkia leo.

Wacheza samba timu ya taifa ya Brazil walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ecuador mshambuliaji Neymer junior, aliipatia timu yake bao la kwanza kwa penati beki wa kushoto wa Ecuador Walter Ayovi, akajifunga kisha kinda Gabriel Jesus, akihitimisha bao la ushindi kwa brazil.
Argentina nao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Urugway bao hilo likuwekwa kambani na mshambuliaji wao mahiri Lionel Messi.
Wekundu weupe wa Paraguay nao wakaibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chile La Roja magoli ya Paraguay yakifungwa na Oscar Romero na beki Paulo da Silva huku bao pekee la Chile likifungwa na kiungo Arturo Erasmo Vidal.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...