30 August, 2016

Kampuni ya Apple kulipa kodi iliokwepa Ireland

Kampuni ya teknolojia ya Apple

Tume ya Ulaya inatarajiwa kuamrisha kampuni kubwa ya teknolojia ya Apple kulipa mabilioni ya dola kama kodi iliyokwepa kulipa.
Hii inafuatia uchunguzi uliofanywa kubainisha makubaliano kuhusu kodi kati ya kampuni hiyo na serikali ya Ireland.
Tume ya Ulaya imewalalamikia mawaziri wa Ireland kwa kuipa Apple kandarasi inayoondoa kodi kwa makubaliano ya kutoa ajira kwa raia wa nchi hiyo.
Apple imesisitiza kwamba hakukua na muafaka maalum, na kwamba inalipa kodi kubwa nchini Marekani ambapo makao yake makuu yapo.
Kampuni ya Apple ni moja ya mashirika ya Marekani yanayolengwa na Tume ya Ulaya kutokana na mikataba yake ya kodi.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...