29 August, 2016

Wanasayansi wanasema maji ya dunia yanahama

Ramani ya dunia
Wanasayansi wametumia picha za za setilaiti kuchunguza namna maji ya dunia yalivyohama kwa zaidi ya miaka 30. 

Walibaini kwamba kilo mita za mraba 115,000 za ardhini kwa sasa zimefunikwa na maji na kilomita 173,000 za maji zimefunikwa sasa na ardhi.
Ongezeko kubwa la maji limetokea katika eneo tambarare la betan , huku bahari ya Aral eneo kubwa la maji sasa limegeuka kuwa ardhi.
wanasayansi hao wanasema kuwa maeneo ya mwambao pia yamekuwa na mabadiliko makubwa .
Utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Deltares ya nchini Uholanzi umechapishwa na jarida la mabadiliko ya asili ya hali ya hewa. Tibetan Plateau
Watafiti walitathmini picha za setilaiti azilizochukuliwa na kituo cha wataalam wa masuala ya anga cha Nasa ,ambacho kimekuwa kikichunguza dunia kwa miongo kadhaa .
Waliweza kufuatilia mabadiliko ya sehemu ya juu ya dunia inayoweza kuonekana kwenye kipimo maalum .
Waliweza kubaini eneo pana ambalo wakati mmoja liliwahi kuwa ardhi ambalo sasa limekuwa na maji , eneo kubwa zaidi likiwa ni lile la maeneo tambarare yenye vilima ya Tibetambako barafu zilizoyeyuka zinasababisha maziwa makubwa .Korea kaskazini
Kuongezeka kwa idadi ya mabwawa pia kunaongeza kiwango cha maji, na kwa kutumia data za setilaiti , Timu hiyo ya wanasayansi iliweza kugundua shughuli za ujenzi ambazo hazikuripotiwa awali.
Dr Fedor Baart kutoka taasisi ya Deltares anasema : "Tulianza kuangalia kwenye maeneo ambayo hayakuwekwa kwenye ramani awali.
"Tulifahamu nchini Myanmar kwamba mabwawa kadhaa yalikuwa yanajengwa, lakini tuliweza kuona mengi . Na pia tuliweza kuona Korea kaskazini na tukaona mabwawa yanayojengwa huko karibu tu na mpaka wa Korea Kusini." bahari ya Aral
Vile vile watafiti waliweza kubaini kwamba hata maeneo makubwa ya maji yamebadilika kuwa ardhi sasa
Mabadiliko haya makubwa yalionekana katika bahari ya Aral Sea katika Asia ya kati.
Yale yaliyowahi wakati mmoja kuwa maziwa makubwa duniani kwa sasa karibu yanakauka kabisa baada ya wahandisi kuelekeza maji katika shughuli za kilimo cha umwagiliaji.

CHANZO: BBC 

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...