18 May, 2016

Japo utaumia lakini Utajifunza.

 

Wakati mwingine inatokea hali ya sisi kujichukulia kwamba na watu walio shindwa na kukata tamaa, ila hakuna ukweli juu ya jambo hili. Ni lazima tupitia mchakato mzima wa maisha ili tuweze kuishi maisha yanayo stahili. Na mchakato huu huja pale tunapo jaribu kufanya vitu mbali mbali kwa wakati tofauti tofauti, na Huo ndio ukweli wa maisha. Ni lazima tupige mawazo hasi katika maisha . 

Labda hii inatokana na sisi kutotambua ni maana ya Neno "Kushindwa" kwa sababu ndani yake hakueleweki. Lakini wacha nikuambie kitu kimoja, Kila jambo nililo fanikiwa nilifanikiwa kupitia Kushindwa lakini sikukata tamaa.

Failure isn’t fatal, but failure to change might be” – John Wooden

Ninacho zungumzia mimi ni kwamba, yatupasa kuchukulia neno "Kusindwa" kama darasa la kujifunzia. Lichukulie neno 'Kushindwa' na kulileuza kuwa 'Kujifunza'. Najua ni Ngumu kufanya hivyo ila ndio njia nzuri ya kufanikiwa, inaumiza ila mafanikio yako ndiko yaliko. 

“Success is most often achieved by those who don’t know that failure is inevitable.” – Coco Chanel

Subiri kidogo nikupe kitu hapa..

  Nilimuuliza Girlfriend wangu ni nini maana ya Kushindwa, na akanijibu kwa kifupi "Ni kufika mwisho" ndio ni kufika mwisho ndipo nilipo chukua Computer yangu na kutafuta maana halisi ya kushindwa. Nikapata kama ifutavyo. Niliandika What really is “failing”?

Unaona hii? A wekness in a character! Kushindwa(maungufu/weakness) kunaweza kuimarishwa kwa kufanya zaidi(Practice enough). Kushindwa siyo njia ya kufikia tamati ya maisha, Kushindwa ni jambo zuri mno katika maisha maana utapata akili mpya ya na kuzidi kupambana.

“Only those who dare to fail greatly can ever achieve greatly.” – Robert F. Kennedy

 Hapa nimekuwekea mambo machache ambayo mara nyingi huwa tuna "shindwa" lakini tukiweka nguvu na akili zetu huwa tuna fanikiwa kweli kweli:-

1.Utashindwa katika urafiki.

Marafiki milele? laa hasha. Itafika kipindi rafiki ulio nao utawaona wamebadilika yaani wamekua tofauti na ulivyo tegemea. Inauma kwa kweli lakini ni jambo ambalo tunapaswa kulipitia kama wanadamu, wapo marafiki zako watakudanganya, wengine watakukimbia katika matatizo uliyo nayo na wengine watakuambia majukumu yamezidi hivyo hawana muda na wewe na maambo mengi ilimradi wakutenge ( Doh!) lakini unapaswa kujifunza jambo katika hili. Chagua marafiki sahihi na wa kweli, ambao hata ukianguka popote mbali na wao watakutafuta na kukuokota. Achana na marafiki wote unao ona ni wanafiki(Najua ina umiza ila yakupasa kufanya hivyo). Usiogope maana baada ya hili utakua muwazi na huru daima na mwisho wa siku utashinda. 

“The phoenix must burn to emerge.” – Janet Fitch

 2.Utashindwa Kufanya maamuzi Makubwa.

Nikiwa mwenye umri wa mika 20 na kitu hivi mpaka sasa nashindwa kueleza ni maamuzi magumu mangapi nimekwisha kushindwa kuyachukua. Hapana itakuwa ni Hatari kwa mimi kuyataja hapa yote. Nitaangalia machache kwa ajili yako. Lakini point ni kwamba hasa pale unapokuwa una ukosa mwongozo wa mtu fulani muhimu katika maisha yako, unakuwa unafanya maamuzi ya ajabua mabayo mwishoni unakuja kuyajutia. Pointi moja ya kweli ni kwamba utakua umeshindwa kuiruhusu hali hii ikutokee katika maisha yako na kama hali ni hiyo, basi iwe ni njia yenye maumivu makubwa katika kuelekea kwenye mafanikio yako. 

Tafuta mtu wa kukusaidia, soma mambo mengi yahusuyo maisha(Tumia internet yako vizuri). Hali hii hutokea wengi mno hasa vija ambao wengi wetu ndio tunaanza maisha. Jaribu kuchanganua jambo hili kwa kina.

I’ve failed over and over and over again in my life and that is why I succeed.” – Michael Jordan

3.Utashindwa kuwekeza kwa ajili ya badae.

"Unaishi mara moja tuu" is the mantra of most 20-somethings, hii inaonekana ni nzuri si ndiyo? Muda baada ya muda utafahamu ni nini ambacho uatkifanya kwa undani peke yako. Kumbuka, kama unataka kuwa na familia na kuitunza, basi mahusiano na wapenzi wengi siyo suluhisho. Na ndivyo ianatakiwa kuwa katika malengo yako ya muda mrefu. Utajifunza kuwa mtu wa maono ya mbali.

“Failure should be our teacher, not our undertaker. Failure is delay, not defeat. It is a temporary detour, not a dead end. Failure is something we can avoid only by saying nothing, doing nothing, and being nothing.” – Denis Waitley

4.Utashindwa kuendeleza Muonekano wako(Personal style).

Jamii, familia na marafiki vimetusafisha akili zetu kwa ujumla wake. Pale ambapo tuana mambo na kujaribu kuyabadili, basi tunakua tukijaribu kubadili muonekano wetu.Easier said than done but why not learn about self development? (Jifunze katika hili).

“When you take risks you learn that there will be times when you succeed and there will be times when you fail, and both are equally important.” – Ellen DeGeneres

5.Utashindwa Kupangilia na kumiliki pesa zako.

Wengi walio katika umri wa miaka ya 20 hadi ishirini na ushehe, hawanaga plan yeyote ya kuaminika, na wengi unakuta wako vyuoni wakifanya masomo yao(Wrong Degrees) na wengine wakiwa wamekaa tuu wakingojea Elimu kubadili maisha yao. Ni lazima tutafute njia mbadala kuondokana na hii hali. Na  ndivyo ilivyo kwa Pesa. Huwezi ukaijua pesa ilivyo mpaka ufahamu Lugha ya pesa. Chakufanya hapo ni kununua vile vitu vya muhimu, kuwekeza katika jambo moja tuu ambalo baade litakuja kukupa uhuru wa maendeleo. Usihangaike kununua vitu ambavyo utanunua leo na kutumika leo na kesho itakavyo fika utajikuta huna. 

“I have not failed. I’ve just found 10,000 ways that won’t work.” – Thomas A. Edison

 Yapo mengi utakayo shindwa kufanya katika maisha ila kama utapambana kwa nguvu zako zote na akili zako zote, hakika utaweza kuyashinda, Japo utakua umeumia ila utakua umeupata Ushi.



No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...