09 April, 2016

Amani ya Moyoni mwako ndio Kunawiri kwa Uso wako.

Awali ya yote nipende kumshukuru Mungu Wangu aliye Juu kwa kunifikisha hapa nilipo maana siyo kwa uwezo wangu ama kwa ujanja wangu kufika hapa nilipo bali ni Kwa neema tuu.
Baada ya shukrani zangu za pekee kwa Mwenyezi Mungu, basi nichukue muda Huu kukushkuru wewe Mdau na Msomaji wa Makala Tofauti tofauti hapa MTOKAMBALI,

Leo nitazungumzia Mambo kadhaaa Juuu ya Maisha ya kila siku, na nmekuongoza na kichwa cha habari Tanjwa hapo juu na Hiyo ndio mada ama point kuu katika hili.

Ngoja nikuulize swali rahisi; Furaha yako ni nn? ni nini chanzo cha Furaha hiyo? na Ni sehemu gani ya mwili wako hutumika kuhifadhi Furaha hiyo? Utanijibu maswali hayo kwenye Box la maoni hapo chini ila kwa sasa Tusonge mbele katika mada yetu ya Leo.

  Niliwahi kukutana na rafiki yangu kipenzi ambae tuliachana kwa muda mrefu kutokana na Masomo ambapo tuliachana tangu Tukiwa na Umri wa miaka 10 huko jijini Arusha, kwa kweli nilistuka kumuona Rafiki yangu huyo licha ya furaha yakumtia tena machoni baada ya muda mrefu kukaa bila kuonana.
Hakika sura yake ilionekana kukomaa mithili ya MZEE mwenye umri wa mika 90, licha ya Mali nyingi na Maisha mazuri aliyokuwa nayo Rafiki huyo lakini kwa kweli sura yake haikuendana na Umri pamoja na mali alizonazo.
  Niliamua kwenda na Rafiki huyo katika Restaurant moja maarufu ili kupata angalao kinywaji na kufahamu mengi yaliyotokea kati yetu kipindi ambacho tuliachana. Baada ya hapo niliamua Kumuuliza kunani Rafki yangu kuonekana na sura ya mzee angali wewe ni kijana mdogo? je ni Mvinyo umekufanya hivyo ama nini?

Jibu alilonijibu lilikua kama ifutavyo.Wewe acha tuu ndugu yangu moyoni mwangu sina Amani kabisa.
Nikamuuliza tena kwa nini?
Ndipo akaniambia Ndugu yangu maisha ya Ujana yana mengi, usipokua makini utajikuta katika hali kama yangu licha ya mali na mafanikio makubwa utakayopata kutokana na kazi za mikono yako. Niliwaki kuwa na Mwanamke mmoja ambae tulikutana nae chuoni na tukapendana kisha baada ya masomo niliamua kufunga nae ndoa na kwa kweli maisha yalikua mazuri na tulifanikiwa kuwa na watoto mapacha mmoja wa kiume na mmoja wa kike, ilikua ni furaha isiyokua na kifani, ila huwezi kuamini furaha hiyo iliingia doa pale ambapo mwanamke huyo alipoamua kutoroka na kuniachia watoto hao wakiwa na umri wa miezi miwili tuu! mpaka leo sifahamu yuko wapi, yuko hai ama mfu, nmemtafuta kila mahali ila nimegonga mwamba sasa jambo hili limekua likiutesa moyo wangu kila kukicha.

Mpaka hapo utakua umepata picha nini hasa kilichofanya sura ya Rafiki huyo kipenzi kuonekana kama mzee. Nilipata jibu sahihi kwamba Amani ya moyo wa mtu ndio kunawiri kwa Uso wake.
Yawezekana kwa namna moja ama ningine ukawana na matatizo kibao ambayo umeyahifadhi moyoni mwako na mbaya zaidi umekosa utatuzi wa matatizo hayo.

Leo nakushauri jaribu kuondoa matatizo hayo moyoni mwako kwa kutafuta suluhisho sahihi, siku hizi zipo njia nyingi la mambo hayo jaribu kufanya hivyo ili kuondokana na mabo yasiyo na ulazima. Ya nini kuishi katika matatizo ilhali maisha haya ya leo Mafupi?
Tafakari.



PITIA NA HIZI PIA 
 1.Oliver Mtukudzi picha Halisi ya Muziki wa Kiafrica. 

2. Wafahamu madancer Albir Rojas na Sara Lopez wakali wa 'Kizomba dance'

3.Mfahamu R.KELLY na maisha yake ya Muziki kiujumla

 .> LIFAHAMU KABILA LA HADZABE KABILA PEKEE LINALOISHI KWA

 >KIJANA BADILI MTAZAMO WAKO NA JENGA MAISHA BORA

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...