06 April, 2016

Mfahamu John Lennon na Historia nzima ya Kundi La The Beatles

Kama wewe ni mpenzi wa Burudani ya Muziki basi hapa nitakua nimekukuna Moyo wako maana utakua unafahamu naongelea nini leo. Leo nitazungumzia Juu ya Kundi hili nguli la Muziki aina ya "ROCK" kutokea mitaa ya Liverpool nchini Uingereza.


 The Beatles ni Kundi NGULI  la Muziki kuwahi kutokea katika ulimwengu wa muziki ambapo kundi hilo liliundwa mnamo mwaka 1960 huko jijini Liverpool nchini Uingereza chini ya Uongozi wa John Lennon ambapo kundi hili lilifanikiwa kuufanya Muziki aina ya ROCK kuwa wa thamani na hata kufanya biashara.


    Waliweza kutengeneza vibao kama vile  "Yesterday, "Hey Jude," "Penny Lane, "With A Little Help From My Friends," "Norwegian Wood (This Bird Has Flown)," "Day Tripper" and "Come Together."Ambapo vibao hivyo na umahiri wao viliifanya bendi hiyo kuwa bandi maarufu na yenye nguvu kwa muda wote.

 wahusika wa kundi hilo walikua ni John Lennon, Paul McCartney, George Harrison na Ringo Starr.


 John Lennon

John LennonJohn Lennon alizaliwa mnamo October 9, 1940 huko jijini Liverpoll , jina lake kamili alijulikana kama John Winston Lennon ambapo wengi ndio tunaemtambua kuwa ndie mwanzilishi wa kundi hilo. Akiwa na umri wa miaka 4 wazazi wake waliachana na kumfanya John kuishi na shangazi yake aliyejulikana kwa jina la MIMI


 Alikua ni mwandishi wa mashairi na muimbaji katika kundi hilo na alifanikiwa kusoma katika chuo cha sanaa huko Jijini liverpool kiitwachwo Liverpool college of Arts.


Mnamo mwaka 1957 John Lennon Alikutana na Paul McCartney na kumuomba Paul kujiunga na na kundi lake la muziki  ambalo teyari alikua nalo lililokwenda kwa jina la Quarry Men na walifanikiwa kuwa na uhusiano mzuri katika uandishi wa ngoma kali. Mnamo mwaka 1969 baadae aliondoka katika kundi hilo na nakufanya kazi na mke wake Mjapani  aliyejulikana kwa jina la Yoko Ono pamoja na waimbaji wengine waliokua njee ya The Beatles. John Lennon aliuawa mnamo December 8, 1980 na  shabiki wake ambae alikua kichaa.


Hiyo ni historia fupi ya Mwanzilisi wa Kundi la The Beatles japo kwa uchache wake,

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...