25 March, 2016

Huyu ndiye Samuel Eto’o Fils

 


Jina Samuel Eto'o, sio jina ngeni masikioni mwa Tulio wengi. Ni mzaliwa wa Africa Magharibi katika nchi ya Cameroon na alizaliwa mnamo March 10, 1981. Ni mmoja kati ya wachezaji maarufu na wenye mafanikio makubwa mno barani Africa na Ulimwengini kote.
Eto'o Alijiunga na Sports Academy moja Huko nchini iliyojulikana kwa jina la Kadji na alianza kuonekana ama kufahamika kitaifa( cameroon) akiwa anachezea timu ya UCB Douala ililiyokua ikishiriki ligi daraja la pili mnamo mwaka 1996.

Akiwa na Umri wa miaka 16 pekee, aliweza kuwavutia klabu ya Real-Madrid ambao walimpatia mkataba wa kuichezea timu hiyo mnamo mwaka 1997. Eto'o Alichaguliwa kujiunga na timu yake ya taifa katika kikosi kilicho shiriki kombe la dunia mwaka 1998 ambapo  kikosi hicho kilitolewa mapema katika michuano hiyo.
Jina Eto'o lilizidi kukua zaidi na hasa pale alipokua katika michuano ya Mataifa ya Africa alipofumania nyavu mara nne katika mchezo dhidi ya Nigeria mwaka 2000.

Umahiri wake ulizidi kuonekana katika michezo ya Olimpiki mwaka huo huo wa 2000 pale ambapo kwa mara ya kwanza Cameroon waliweza kuwafunga Spain nakuweka historia katika soka nchini humoa, katika mchezo wa Finali michuano ya Olimpiki Cameroon (Indomitable Lions) wakiwa nyuma kwa jumla ya bao 2-0, Eto'o na mchezaji mwenza Patrick Mboma waliweza kusawazisha mabao hayo na kuenda moja kwa moja katika dakika 30 za nyongeza za mchezo huo na hata hivyo timu hizo hazikufungana na hatua ya matuta ikafuatia na hatimae Cameroon wakaibuka washindi.

Alichezea klabu ya Real Madrid hadi mwaka 2000 na ndipo klabu ya  Real Mallorca iliweza kumnunua mchezaji huyo kwa dau la $6.3 millioni ambalo lilikua ni dau kubwa kwa kipindi kile. Akiwa klabuni hapo Real Mallorca, Eto'o alikua mfungaji bora wa timu hiyo kwa kipindi chote na kuweka historia katika klabu hiyo ingawaje timu hiyo haikuwa na mafanikio makubwa katika ligi ya Spanish. Etoo aliiongoza tena Cameroon katika michuano ya Mataifa ya Africa na Kombe la Dunia mnamo mwaka 2002.

Eto'o alisaini mkataba na club ya FC Barcelona mnamo mwaka 2004 na hulo alizidi kung'ara. Alishinda rekodi yake ya tatu mfululizo akiwa mchezaji bora wa Africa mwaka 2005. Akiwa na Barcelona alichukua ubingwa ligi kuu na ligi ya mabingwa mnamo mwaka 2005 na mwaka 2006. Mnamo mwaka 2008 Eto'o alitajwa kama mfungaji bora wa muda wote katika michuano ya Mataifa ya Africa pale alipoisaidia timu ya ya taifa katika mchezo wa Fiinali dhidi ya Egypt( a loss to Egypt)

Akiwa na Barcelena aliiwezesha timu hiyo kuchukua makombe makubwa kwa wakati mmoja yaani Kombe la ligi, kombe la Ngao ya Mflame(Copa del Rey), kombe la ligi ya mabingwa Ulaya(Champions League) na lile la mabara(continental championship) hiyo ilikua ni mwaka 2009.  Eto'o alipelekwa kwa mkopo  Inter Milan mwisho wa msimu na kuiwezesha timu hiyo kuchukua kombe la ligi ya Mabingwa mnamo mwaka 2010 na akiwa klabuni hapo alikuwa mfungaji bora kwa jumla ya magoli 37 katika msimu wa 2010-2011.

Mnamo mwaka ulio fuatia Eto'o alisaini mkataba na timu ya Urusi inayoitwa Anzhi Makhachkala, mkataba unaotatwa kuwa ni mkataba mnono katika historia ya soka ulimwenguni na mkataba huo ulikua ni wa mwaka mmoja tuu pekee. Mnamo mwaka 2013 aliingia mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Chelsea ligi kuu uingereza na baadae kujiunga na Everton kabla ya kujiunga na Sampdoria ligi kuu Italia(Serie A) mnamo mwaka 2015.
 Etoo anasema :- The first thing for victory is believing, believing that you can achieve. When you believe that you can achieve something, I'm sure that you're 60 percent on the path to victory. 

Huyo ndio Samuel Eto'o  Fils Mwafrika aliewahi kuvitesa vichwa vya wazungu katika mchezo wa soka.
Kwa maoni na Ushauri kuhusiana na blog hii tafadhali tutumia ujumbe katika anwani zifuatazo:
0767322193
mtokambali2015@gmail.com
Pia tunakukaribisha kuwa mmoja ya waandishi wetu tafadhali tembelea hapa http://mawerenews.blogspot.com/p/blog-page_20.html kujua jinsi ya kujiunga nasi 

Download Music: Yemi Alade - Ferrari

post-feature-image Mwanadada Yemi Katuletea ngoma mpya inayokwenda kwa jina la FERRRI.
Bofya >>>>>> HAPA <<<<< kuudawnlod

Barack Obama Quotes: The Most Inspirational Sayings Of His Presidency

1) On Change:
“Change will not come if we wait for some other person, or if we wait for some other time. We are the ones we’ve been waiting for. We are the change that we seek.” – Barack Obama
change-will-not-come-if-barack-obama
2) On The Importance of Hard Work:
“We need to steer clear of this poverty of ambition, where people want to drive fancy cars and wear nice clothes and live in nice apartments but don’t want to work hard to accomplish these things. Everyone should try to realize their full potential.” – Barack Obama


3) On The Potential Of Americans:
barack-obama-quote-2
 
4) On values:
“If we aren’t willing to pay a price for our values then we should ask ourselves whether we truly believe in them at all” – Barack Obama
file_001

5) On Love:
barack-obama-quote-8

 6) On dizzying celebrity:
I’m so overexposed, I’m starting to make Paris Hilton look like a recluse. – Barack Obama
im-so-overexposed-im-making-paris-barack-obama

7) On Americans Being Able To Make It: barack-obama-quote-3

24 March, 2016

UNALIFAHAMU KUNDI LA UB40?


Ninapoongelea UB40 hapana shaka kwa wewe mpenzi wa burudani ya Muziki utakua unajua anwaongelea wakina nani.  Kwa namna moja ama nyingine utakua umekwisha kusikia kibao kama vile “Red Red Wine, I got the Cup” na ule wa Falling in Love with You. Sasa pata kujua nyimbo zote hizo ni kazi za kundi hili la muziki kutoka huko Kusini mwa Birmingham, England. Kundi hili lilikua na vichwa kama vile Brown, Bria Travers, Trecence Oswald na Norman Hassan

Mwanzo wa kundi hili.
Wana kikundi hicho walikua marafiki tangu wakiwa shuleni na Ugumu wa maisha walio kua nao ndio uliosababisha kuunanisha vipaji vyao na kutengeneza kikundi hicho ili kufanya muziki na kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini waliokua nao.
Jina la Ub40 lilikuja kutokana  na wananchi wa Uingereza kutoa waraka wenye kurasa 40 uliohusu mafao yao ya afya na ajira . hivyo basi kundi hili likaamua lijiite Ub40. 
Brian Travers alijiunga na kundi hilo akiwa na zana yake ya Saxophone huku wengine wakija na magitaa. Na mara walianza kubandika mabango katika mitaa ya Uingereza wakitangaza bendi yao.
 Wimbo wao wa kwanza  ulisikika  katika Ukumbi wa The Hare na Hounds Pub Februari 1979 katika shereh za kuzaliwa rafiki yao. 
Chrissie Hynde ndiye aliye waona vijana hao wakiimba katika ukumbi mmoja ndipo alipoamua kuwafadhili na kuwapa nafasi ya kurekodi wimbo wao wa kwanza “King/Food for Thought” wimbo  ambao ulishika  nafasi ya 4 katika chati za muziki nchini humo.
Albamu yao ya kwanza iliitwa “Signing Off” wakimaanisha wanayamaliza malalamiko yao ya ukosefu wa ajira  na mafao ya afya. Albamu hii ilizinduliwa rasmi Agosti 1980.
Ikumbukwe kua mnamo mwaka 2010 mahakama ya Uingereza ilitangaza kuwa UB40 imefilisika. Kufilisika kwao kumekuja baada ya wanamuziki wane kina Jimmy Brown, Bria Travers, Trecence Oswald na Norman Hassan kushindwa kulipa madeni yao ya kodi.
Kundi hili ndilo kundi linalotajwa kuwahi kuuza nakala nyingi duniani katika nyanja ya Muziki. 

Japo kwa ufupi nmeweza kukupatia historia ya Kundi  hili amabalo liliwika mno miaka ya nyuma.

Kwa maoni na ushauri tafadhali tutumie ujumbe kupitia anwani zifutazo:-
0767322193
mtokambali2015@gmail.com  

New Music: Vanessa Mdee - Niroge (Audio+Video)

post-feature-image Ile ngoma tuliyo kuwa tukiiingoja Kutoka kwa Vee Money "Niroge" hii leo tunayo. Imetengenezwa na NAHREEL
Bofya >>>>>HAPA<<<< kuidownload Pia tizama video yake Hapo chini

Download Music: Jose Chameleone Ft Bob Juniour - Baki Nae

post-feature-image
Muunganiko wa Dr Jose Chamileone mwanamuziki kutokea nchini Uganda ambao wameufanya kwenye Baki Nae na muimbaji wa Bongo Fleva, Bob Junior wa nchini Tanzania.
Bofya >>>>>>>HAPA <<<<<< Kuupata wimbo huo

Download Music: Rudy Ft Wakazi - Sijutii

post-feature-imageMuunganiko wa sauti ya rn'b kutoka kwa Ruby imependezesha pale rapper Wakazi akipitisha mashairi yake kwenye remix ya Sijutii.
Bofya HAPA kuudownload

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...