Jina Samuel Eto'o, sio jina ngeni masikioni mwa Tulio wengi. Ni mzaliwa wa Africa Magharibi katika nchi ya Cameroon na alizaliwa mnamo March 10, 1981. Ni mmoja kati ya wachezaji maarufu na wenye mafanikio makubwa mno barani Africa na Ulimwengini kote.
Eto'o Alijiunga na Sports Academy moja Huko nchini iliyojulikana kwa jina la Kadji na alianza kuonekana ama kufahamika kitaifa( cameroon) akiwa anachezea timu ya UCB Douala ililiyokua ikishiriki ligi daraja la pili mnamo mwaka 1996.
Akiwa na Umri wa miaka 16 pekee, aliweza kuwavutia klabu ya Real-Madrid ambao walimpatia mkataba wa kuichezea timu hiyo mnamo mwaka 1997. Eto'o Alichaguliwa kujiunga na timu yake ya taifa katika kikosi kilicho shiriki kombe la dunia mwaka 1998 ambapo kikosi hicho kilitolewa mapema katika michuano hiyo.
Jina Eto'o lilizidi kukua zaidi na hasa pale alipokua katika michuano ya Mataifa ya Africa alipofumania nyavu mara nne katika mchezo dhidi ya Nigeria mwaka 2000.
Umahiri wake ulizidi kuonekana katika michezo ya Olimpiki mwaka huo huo wa 2000 pale ambapo kwa mara ya kwanza Cameroon waliweza kuwafunga Spain nakuweka historia katika soka nchini humoa, katika mchezo wa Finali michuano ya Olimpiki Cameroon (Indomitable Lions) wakiwa nyuma kwa jumla ya bao 2-0, Eto'o na mchezaji mwenza Patrick Mboma waliweza kusawazisha mabao hayo na kuenda moja kwa moja katika dakika 30 za nyongeza za mchezo huo na hata hivyo timu hizo hazikufungana na hatua ya matuta ikafuatia na hatimae Cameroon wakaibuka washindi.
Alichezea klabu ya Real Madrid hadi mwaka 2000 na ndipo klabu ya Real Mallorca iliweza kumnunua mchezaji huyo kwa dau la $6.3 millioni ambalo lilikua ni dau kubwa kwa kipindi kile. Akiwa klabuni hapo Real Mallorca, Eto'o alikua mfungaji bora wa timu hiyo kwa kipindi chote na kuweka historia katika klabu hiyo ingawaje timu hiyo haikuwa na mafanikio makubwa katika ligi ya Spanish. Etoo aliiongoza tena Cameroon katika michuano ya Mataifa ya Africa na Kombe la Dunia mnamo mwaka 2002.
Eto'o alisaini mkataba na club ya FC Barcelona mnamo mwaka 2004 na hulo alizidi kung'ara. Alishinda rekodi yake ya tatu mfululizo akiwa mchezaji bora wa Africa mwaka 2005. Akiwa na Barcelona alichukua ubingwa ligi kuu na ligi ya mabingwa mnamo mwaka 2005 na mwaka 2006. Mnamo mwaka 2008 Eto'o alitajwa kama mfungaji bora wa muda wote katika michuano ya Mataifa ya Africa pale alipoisaidia timu ya ya taifa katika mchezo wa Fiinali dhidi ya Egypt( a loss to Egypt)
Akiwa na Barcelena aliiwezesha timu hiyo kuchukua makombe makubwa kwa wakati mmoja yaani Kombe la ligi, kombe la Ngao ya Mflame(Copa del Rey), kombe la ligi ya mabingwa Ulaya(Champions League) na lile la mabara(continental championship) hiyo ilikua ni mwaka 2009. Eto'o alipelekwa kwa mkopo Inter Milan mwisho wa msimu na kuiwezesha timu hiyo kuchukua kombe la ligi ya Mabingwa mnamo mwaka 2010 na akiwa klabuni hapo alikuwa mfungaji bora kwa jumla ya magoli 37 katika msimu wa 2010-2011.
Mnamo mwaka ulio fuatia Eto'o alisaini mkataba na timu ya Urusi inayoitwa Anzhi Makhachkala, mkataba unaotatwa kuwa ni mkataba mnono katika historia ya soka ulimwenguni na mkataba huo ulikua ni wa mwaka mmoja tuu pekee. Mnamo mwaka 2013 aliingia mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Chelsea ligi kuu uingereza na baadae kujiunga na Everton kabla ya kujiunga na Sampdoria ligi kuu Italia(Serie A) mnamo mwaka 2015.
Etoo anasema :- The first thing for victory is believing, believing that you can achieve. When you believe that you can achieve something, I'm sure that you're 60 percent on the path to victory.
Huyo ndio Samuel Eto'o Fils Mwafrika aliewahi kuvitesa vichwa vya wazungu katika mchezo wa soka.
Kwa maoni na Ushauri kuhusiana na blog hii tafadhali tutumia ujumbe katika anwani zifuatazo:
0767322193
mtokambali2015@gmail.com
Pia tunakukaribisha kuwa mmoja ya waandishi wetu tafadhali tembelea hapa http://mawerenews.blogspot.com/p/blog-page_20.html kujua jinsi ya kujiunga nasi
No comments:
Post a Comment