24 March, 2016

UNALIFAHAMU KUNDI LA UB40?


Ninapoongelea UB40 hapana shaka kwa wewe mpenzi wa burudani ya Muziki utakua unajua anwaongelea wakina nani.  Kwa namna moja ama nyingine utakua umekwisha kusikia kibao kama vile “Red Red Wine, I got the Cup” na ule wa Falling in Love with You. Sasa pata kujua nyimbo zote hizo ni kazi za kundi hili la muziki kutoka huko Kusini mwa Birmingham, England. Kundi hili lilikua na vichwa kama vile Brown, Bria Travers, Trecence Oswald na Norman Hassan

Mwanzo wa kundi hili.
Wana kikundi hicho walikua marafiki tangu wakiwa shuleni na Ugumu wa maisha walio kua nao ndio uliosababisha kuunanisha vipaji vyao na kutengeneza kikundi hicho ili kufanya muziki na kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini waliokua nao.
Jina la Ub40 lilikuja kutokana  na wananchi wa Uingereza kutoa waraka wenye kurasa 40 uliohusu mafao yao ya afya na ajira . hivyo basi kundi hili likaamua lijiite Ub40. 
Brian Travers alijiunga na kundi hilo akiwa na zana yake ya Saxophone huku wengine wakija na magitaa. Na mara walianza kubandika mabango katika mitaa ya Uingereza wakitangaza bendi yao.
 Wimbo wao wa kwanza  ulisikika  katika Ukumbi wa The Hare na Hounds Pub Februari 1979 katika shereh za kuzaliwa rafiki yao. 
Chrissie Hynde ndiye aliye waona vijana hao wakiimba katika ukumbi mmoja ndipo alipoamua kuwafadhili na kuwapa nafasi ya kurekodi wimbo wao wa kwanza “King/Food for Thought” wimbo  ambao ulishika  nafasi ya 4 katika chati za muziki nchini humo.
Albamu yao ya kwanza iliitwa “Signing Off” wakimaanisha wanayamaliza malalamiko yao ya ukosefu wa ajira  na mafao ya afya. Albamu hii ilizinduliwa rasmi Agosti 1980.
Ikumbukwe kua mnamo mwaka 2010 mahakama ya Uingereza ilitangaza kuwa UB40 imefilisika. Kufilisika kwao kumekuja baada ya wanamuziki wane kina Jimmy Brown, Bria Travers, Trecence Oswald na Norman Hassan kushindwa kulipa madeni yao ya kodi.
Kundi hili ndilo kundi linalotajwa kuwahi kuuza nakala nyingi duniani katika nyanja ya Muziki. 

Japo kwa ufupi nmeweza kukupatia historia ya Kundi  hili amabalo liliwika mno miaka ya nyuma.

Kwa maoni na ushauri tafadhali tutumie ujumbe kupitia anwani zifutazo:-
0767322193
mtokambali2015@gmail.com  

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...