13 July, 2015

Baada ya muigizaji mrembo wa filamu za Bongo, Elizabeth “Lulu” Michael kuandika tweet iliyotafsiriwa kuwa huenda ni kijembe kwa mrembo fulani, amefafanua alichokimaanisha.

Lulu amesema kuwa alichokiandika kwenye post hiyo ilikuwa ni utani, na wakati huo huo kukubali kuwa inaweza kuwa na ukweli ndani yake.

It was a joke, but sort of ukweli pia kwa sababu mara nyingi kumekuwa na dhana watu wa nje wanachukulia kama vile viti maalum ni vya kupeana” alisema kupitia The Playlist ya Times Fm.

Hiki ndicho alipost:
 Lulu aliendelea kwa kusema:
…probably watu wameichukulia kama nimemsnitch mtu, mimi siko hivyo na sinaga hayo mambo kabisa. Ni kwamba nimefanya kama utani, lakini watu wasichukulie poa kwamba kila anaewekwa pale kwamba ana sura nzuri, kila anaewekwa pale ana umbo zuri.

video mpya: “Applaudise!” Iyanya

iyaaanya2
Msanii maarufu kutoka Nigeria Iyanya anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za burudani. Baada ya kudondosha video ya Nakupenda alioshirikiana na Bongo Superstaa Diamond Platnumz leo hii amerudi na kichupa kipya.
iyaanya
Wimbo unaitwa  Applaudise na hapa chini nimekusogezea video yake. Bonyeza play kuitazama.

Diamond Platnumz akibusu tumbo la Zari, natamani mjue jinsi navyompenda Zari.

Staa wa ‘Nana’ Ft Mr Flavour Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa anatamani watu wajue jinsi anavyompenda Zari Tlale aka Zari The Boss Lady.
Kama wewe ni shabiki basi ni hii ni nafasi yako ya kujua kuwa wapenzi hawa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza mwezi ujao.
Screenshot_2015-07-13-10-28-43 Screenshot_2015-07-13-10-28-47 Screenshot_2015-07-13-10-29-06 Screenshot_2015-07-13-10-29-28 Screenshot_2015-07-13-10-29-34 Screenshot_2015-07-13-10-29-40

Trey Songz kwenye headlines na hii ‘About You’…(Video)

treysMkali wa R&B Trey Songz amerudi kwenye headlines na ngoma yake mpya inayoitwa ‘About You’, inayopatikana katika albamu yake mpya ya TRIGGA Reloaded

YANGA v GOR MAHIA JUMAMOSI KAGAME KIINGILIO HELA YA MBOGA TU!

CECAFA Chairman Leodegar Tenga (c) Secretary general Nicholas mUSONYE (L) and tff chairman Jamal Malinzi at press conference in DAR yesterdayMichuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Kagame Cup) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi tarehe 18 Julai 2015 jijini Dar es salaam, kwa kushirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na kati.
 Mashindano ya CECAFA Kagame Cup ni mashindano makongwe barani Afrika ambayo yalianza mwaka 1967 kwa kushirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na mwaka huu ni mashindano ya 40 tangu kuanza kwa michuano hiyo
Klabu ya Simba ndio timu inayoongzoa kwa kutwaa ubingwa huo mara sita (6) ikifuatiwa na Yanga, Gor Mahia zilizotwa mara (5), APR ya Rwanda ikiwa imetwaa ubingwa huo mara tatu (3). Yanga na Gor Mahia zina nafasi ya kufikia Simba SC endapo zitafanikiwa kutwaa Ubingwa msimu huu.
Mechi ya ufunguzi ufunguzi siku ya jumamosi uwanja wa Taifa itawakutanisha APR ya Rwanda dhidi ya Al Shandy ya Sudan saa 8 kamili mchana, KMKM kutoka Visiwani Zanzibar watacheza dhidi ya Telecom ya Djibout  uwanja wa Karume saa 10 jioni, huku wenyeji timu ya Yanga wakiwakaribisha Gor Mahia kutoka Kenya saa 10 jioni.
Kuelekea kwenye mashindano hayo, waandaaji wa michuano hiyo CECAFA kwa kushirikiana na wenyeji Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya michezo hiyo, ambapo Uwanja wa Karume kiingilio kitakuwa shilingi elfu mbili (2,000) na uwanja wa Taifa kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu tano (5,000) na kiingilio cha juu ni elfu 20,000 (20,000).
Timu zinazoshiriki michuano hiyo
Kundi A: Yanga (Tanzania Bara), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan).
Kundi B: APR (Rwanda), Al-Shandy (Sudan),LLB AFC (Burundi), Heegan  FC (Somalia).
Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda).
Michuano hiyo ya CECAFA Kagame Cup itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha Supersport.


KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED KINACHOENDA PRE-SEASON CHATAJWA…

CJy6fYyWcAABXyM
Manchester United imetangaza kikosi kinachoenda katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya ‘pre-season tour party’ nchini Marekani na Stori kubwa ni kuchaguliwa kwa golikipa wa mashetani hao wekundu, David De Gea.
Licha ya muendelezo wa tetesi za kutimka Old Trafford kwenda Real Madrid majira haya ya kiangazi, De Gea mwenye miaka 24 amejumuishwa kwenye kikosi hicho, huku Golikipa namba mbili wa United, Victor Valdes akiachwa kwenye orodha hiyo.
Kukosekana kwa Valdes kumewashangaza wengi na kuongeza tetesi kwamba anaweza kuondoka klabuni hapo.
Wachezaji wapya waliosajiliwa Memphis Depay, Morgan Schneiderlin, Matteo Darmian na Bastian Schweinsteiger  wamejumuishwa pia.
Wachezaji wengine walioachwa kwenye kikosi ni Angel Di Maria na Marcos Rojo (ambao wote walicheza Copa America). Pia mlinzi wa kulia Rafael ameachwa.
Man United wanakwenda kushiriki kombe la Mabingwa wa Kimataifa ambapo Kikosi hicho  cha Van Gaal kitacheza mechi nne Marekaini dhidi ya Club America, MLS side San Jose Earthquakes na miamba ya Ulaya Barcelona na PSG.

12 July, 2015

Wizkid na Drake wanayo furaha kukuletea ‘Ojuelegba’ Remix…(Audio)

dreeeSiku chache zilizopita kulikua na taarifa za staa wa Nigeria Wizkid kufanya remix ya ngoma yake ya ‘Ojuelegba’ na staa wa muziki Marekani Drake.
Wawili hao wameungana pamoja na kutuletea collabo ya wimbo huo.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...