Manchester United imetangaza
kikosi kinachoenda katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya ‘pre-season
tour party’ nchini Marekani na Stori kubwa ni kuchaguliwa kwa golikipa
wa mashetani hao wekundu, David De Gea.
Licha ya muendelezo wa tetesi za
kutimka Old Trafford kwenda Real Madrid majira haya ya kiangazi, De Gea
mwenye miaka 24 amejumuishwa kwenye kikosi hicho, huku Golikipa namba
mbili wa United, Victor Valdes akiachwa kwenye orodha hiyo.
Kukosekana kwa Valdes kumewashangaza wengi na kuongeza tetesi kwamba anaweza kuondoka klabuni hapo.
Wachezaji wapya waliosajiliwa Memphis Depay, Morgan Schneiderlin, Matteo Darmian na Bastian Schweinsteiger wamejumuishwa pia.
Wachezaji wengine walioachwa
kwenye kikosi ni Angel Di Maria na Marcos Rojo (ambao wote walicheza
Copa America). Pia mlinzi wa kulia Rafael ameachwa.
Man United wanakwenda kushiriki
kombe la Mabingwa wa Kimataifa ambapo Kikosi hicho cha Van Gaal
kitacheza mechi nne Marekaini dhidi ya Club America, MLS side San Jose
Earthquakes na miamba ya Ulaya Barcelona na PSG.
No comments:
Post a Comment