19 September, 2016

VideoMPYA: Diamond Platnumz na Rayvanny-‘Salome’


Wakali kutokea kiwanda cha Bongofleva Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz pamoja na Raymond a.k.a Rayvanny wakitokea katika Laber ya WCB wametuletea Video yao mpya walio iachia hapo jana September 18 2016. Bofya Play hapo chini kuitizama Video hiyo.

Jonas Mkude amesema kila mechi iliyopo mbele yao ni sawa na fainali

img_0095
Kiungo na nahodha wa Simba Jonas Mkude amesema kila mechi iliyopo mbele yao ni sawa na fainali kwasababu wamepania kufanya vizuri kwenye ligi msimu huu licha ya kuwepo na upinzani mkubwa kwenye ligi.

“Kila mechi kwetu ni fainali, kwa jinsi ligi ilivyo sasahivi, hatuwezi kukubali kutoka suluhu wala kupoteza pointi tatu”, amesema Mkude baada ya kuisaidia timu yake kushinda mbele ya Azam FC.

Nilipotaka kujua nini siri ya ushindi wao katika mchezo wa jana, Mkude alisema: “Siri ya ushindi ni mazozi na mbinu za mwalimu wetu ndiyo zimetuwezesha kupata ushindi dhidi ya Azam.”
Ligi ni ngumu tunaomba mashabiki waendelee kutusapoti tuendelee kufanya vizuri.

ICARDI, PERISIC, WAVUNJA REKODI YA JUVE SERIE A

1
Inter Milan walitoka nyuma na kuwatandika Juventus katika mchezo mkali na wa kusisimua wa derby d’Italia.

Stephan Lichtsteiner aliwapa Juve goli la uongozi dakika ya 66 baada ya kuunganisha krosi nzuri kutoka kwa Alex Sandro.

Hata hivyo, baadaye Mauro Icardi aliswazisha bai kwa wenyeji wa mchezo huo Inter Milan dakika mbili baadaye kwa kuunganisha kwa umahiri mkubwa mpira wa kona.

Ivan Perisic, ambaye aliingia akitokea benchi aliwapa Inter bao la pili kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Icardi, and Juve, huku Gonzalo Higuain ambaye pia aliingia kutokea bechi akishindwa kufurukuta ili kuisawazishia timu yake bao
Mchezaji wa Inter Milan Ever Banega alipewa kadi nyekundu dakika ya tisini.

Matokeo hayo yanafanya Juve kupoteza mchezo wake kwa mara pili kwenye Serie A tangu walivyofungwa bao 1-0 na Sassuolo 28 October, 2015.

Kipigo hicho pia kinamaanisha kwamba Mabingwa Watetezi hao wanashuka mpaka nafasi ya pili nyuma ya Napoli, wakati Inter wakijisogeza mpaka nafasi ya sita.


Source/Chanzo: shaffihdauda.co.tz

Nguli wa muziki Afrika Kusini Mandoza afariki dunia

Mandoza

Nguli wa muziki nchini Afrika Kusini, Mduduzi Tshabalala, al-maarufu Mandoza, amefariki baada ya kuugua saratani kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 38.

Mandoza alisifika kwa albamu kadha za muziki aina ya Kwaito, aina ya muziki wa Afrika Kusini ambao hukaribiana sana na Hip Hop.MandozaNyimbo zake nyingi sana zilivuma, zikiwemo nyimbo kutoka albamu yake ya kwanza Nkalkatha. Familia ya Mandoza imesema mwanamuziki huyo aligunduliwa kuwa na saratani baada ya kuanza kuumwa na kichwa sana pamoja na kutatizwa na macho mwaka mmoja uliopita.

Game of Thrones yatawala tena tuzo za Emmy


Filamu ya televisheni ya Game of Thrones kwa mara nyingine imezoa tuzo nyingi katika tuzo kuu za vipindi vya televisheni Marekani, Emmy.

Washindi wa tuzo hizo wametangazwa katika hafla iliyofanyika mjini Los Angeles.
Mwendelezo huo wa filamu umeshinda tuzo kumi na mbili za Emmys, zikiwemo tuzo za uelekezi bora na utunzi bora wa hadithi.

Mshindi mwingine mkuu amekuwa kipindi cha ucheshi wa siasa 'Veep,' huku Julia Louis-Dreyfus akishinda tuzo yake ya tano mtawalia ya Emmy kwa uigizaji wake kama makamu wa rais wa Marekani.

Game of Thrones
Filamu ya The People versus OJ Simpson inayoangazia uhalifu nayo imeshinda tuzo tisa za Emmy.
Filamu hiyo huangazia kesi mbili za mauaji pamoja na kuondolewa makosa kwa nyota wa zamani wa soka Marekani Orenthal James "O. J." Simpson.

Paralympics yafungwa kwa mbwembwe Rio De Janeiro

Bahman Golbarnezhad
Mashindano ya Olympic kwa walemave mjini Rio De Janeiro, yamemalizika usiku wa kuamkia leo kwa shamrashamra mbalimbali.

Tangazo la kukumbuka ya kufariki kwa mmoja wa wanamichezo Bahman Golbarnezhad, kutoka nchini Iran, lilileta simanzi pia.

Katika michezo hiyo, China imejizolea medali 239, ikifuatiwa na Uingereza 147, na ya tatu ni Ukraine 117.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, Kenya inaongoza kwa kubeba jumla ya medali 6 na Uganda Medali 1.

18 September, 2016

Download Audio Mpya Kutoka kwa Diamond Plutnum Ft Raymond - Salome

Hii ni ngoma Mpya Kutoka kwa Diamong Plutnum akimshirikisha vyema Raymond.. Ngoma imepewa jina la Salome na imefanyiwa Mixing na Producer Laizer. Ngoma hii ina VerSaion Mbili yaani Traditional Version na Club banggers Version.
Bofya DOWNLOAD hapo chini Kuupakua wimbo Huo. DOWNLOAD pia na Club Banngers Version hapo chini

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...