19 September, 2016

Jonas Mkude amesema kila mechi iliyopo mbele yao ni sawa na fainali

img_0095
Kiungo na nahodha wa Simba Jonas Mkude amesema kila mechi iliyopo mbele yao ni sawa na fainali kwasababu wamepania kufanya vizuri kwenye ligi msimu huu licha ya kuwepo na upinzani mkubwa kwenye ligi.

“Kila mechi kwetu ni fainali, kwa jinsi ligi ilivyo sasahivi, hatuwezi kukubali kutoka suluhu wala kupoteza pointi tatu”, amesema Mkude baada ya kuisaidia timu yake kushinda mbele ya Azam FC.

Nilipotaka kujua nini siri ya ushindi wao katika mchezo wa jana, Mkude alisema: “Siri ya ushindi ni mazozi na mbinu za mwalimu wetu ndiyo zimetuwezesha kupata ushindi dhidi ya Azam.”
Ligi ni ngumu tunaomba mashabiki waendelee kutusapoti tuendelee kufanya vizuri.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...