19 September, 2016

Game of Thrones yatawala tena tuzo za Emmy


Filamu ya televisheni ya Game of Thrones kwa mara nyingine imezoa tuzo nyingi katika tuzo kuu za vipindi vya televisheni Marekani, Emmy.

Washindi wa tuzo hizo wametangazwa katika hafla iliyofanyika mjini Los Angeles.
Mwendelezo huo wa filamu umeshinda tuzo kumi na mbili za Emmys, zikiwemo tuzo za uelekezi bora na utunzi bora wa hadithi.

Mshindi mwingine mkuu amekuwa kipindi cha ucheshi wa siasa 'Veep,' huku Julia Louis-Dreyfus akishinda tuzo yake ya tano mtawalia ya Emmy kwa uigizaji wake kama makamu wa rais wa Marekani.

Game of Thrones
Filamu ya The People versus OJ Simpson inayoangazia uhalifu nayo imeshinda tuzo tisa za Emmy.
Filamu hiyo huangazia kesi mbili za mauaji pamoja na kuondolewa makosa kwa nyota wa zamani wa soka Marekani Orenthal James "O. J." Simpson.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...