19 September, 2016
VideoMPYA: Diamond Platnumz na Rayvanny-‘Salome’
Wakali kutokea kiwanda cha Bongofleva Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz pamoja na Raymond a.k.a Rayvanny wakitokea katika Laber ya WCB wametuletea Video yao mpya walio iachia hapo jana September 18 2016. Bofya Play hapo chini kuitizama Video hiyo.
Jonas Mkude amesema kila mechi iliyopo mbele yao ni sawa na fainali
Kiungo na nahodha wa Simba Jonas Mkude amesema kila mechi iliyopo mbele yao ni sawa na fainali kwasababu wamepania kufanya vizuri kwenye ligi msimu huu licha ya kuwepo na upinzani mkubwa kwenye ligi.
“Kila mechi kwetu ni fainali, kwa jinsi ligi ilivyo sasahivi, hatuwezi kukubali kutoka suluhu wala kupoteza pointi tatu”, amesema Mkude baada ya kuisaidia timu yake kushinda mbele ya Azam FC.
Nilipotaka kujua nini siri ya ushindi wao katika mchezo wa jana, Mkude alisema: “Siri ya ushindi ni mazozi na mbinu za mwalimu wetu ndiyo zimetuwezesha kupata ushindi dhidi ya Azam.”
Ligi ni ngumu tunaomba mashabiki waendelee kutusapoti tuendelee kufanya vizuri.
ICARDI, PERISIC, WAVUNJA REKODI YA JUVE SERIE A
Inter Milan walitoka nyuma na kuwatandika Juventus katika mchezo mkali na wa kusisimua wa derby d’Italia.
Stephan Lichtsteiner aliwapa Juve goli la uongozi dakika ya 66 baada ya kuunganisha krosi nzuri kutoka kwa Alex Sandro.
Hata hivyo, baadaye Mauro Icardi aliswazisha bai kwa wenyeji wa mchezo huo Inter Milan dakika mbili baadaye kwa kuunganisha kwa umahiri mkubwa mpira wa kona.
Ivan Perisic, ambaye aliingia akitokea benchi aliwapa Inter bao la pili kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Icardi, and Juve, huku Gonzalo Higuain ambaye pia aliingia kutokea bechi akishindwa kufurukuta ili kuisawazishia timu yake bao
Mchezaji wa Inter Milan Ever Banega alipewa kadi nyekundu dakika ya tisini.
Matokeo hayo yanafanya Juve kupoteza mchezo wake kwa mara pili kwenye Serie A tangu walivyofungwa bao 1-0 na Sassuolo 28 October, 2015.
Kipigo hicho pia kinamaanisha kwamba Mabingwa Watetezi hao wanashuka mpaka nafasi ya pili nyuma ya Napoli, wakati Inter wakijisogeza mpaka nafasi ya sita.
Source/Chanzo: shaffihdauda.co.tz
Nguli wa muziki Afrika Kusini Mandoza afariki dunia
Nguli wa muziki nchini Afrika
Kusini, Mduduzi Tshabalala, al-maarufu Mandoza, amefariki baada ya
kuugua saratani kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 38.Mandoza alisifika kwa albamu kadha za muziki aina ya Kwaito, aina ya muziki wa Afrika Kusini ambao hukaribiana sana na Hip Hop.
Game of Thrones yatawala tena tuzo za Emmy
Filamu ya televisheni ya Game of
Thrones kwa mara nyingine imezoa tuzo nyingi katika tuzo kuu za vipindi
vya televisheni Marekani, Emmy.
Mwendelezo huo wa filamu umeshinda tuzo kumi na mbili za Emmys, zikiwemo tuzo za uelekezi bora na utunzi bora wa hadithi.
Mshindi mwingine mkuu amekuwa kipindi cha ucheshi wa siasa 'Veep,' huku Julia Louis-Dreyfus akishinda tuzo yake ya tano mtawalia ya Emmy kwa uigizaji wake kama makamu wa rais wa Marekani.
Filamu ya The People versus OJ Simpson inayoangazia uhalifu nayo imeshinda tuzo tisa za Emmy.
Filamu hiyo huangazia kesi mbili za mauaji pamoja na kuondolewa makosa kwa nyota wa zamani wa soka Marekani Orenthal James "O. J." Simpson.
Paralympics yafungwa kwa mbwembwe Rio De Janeiro
Mashindano ya Olympic kwa walemave mjini Rio De Janeiro, yamemalizika usiku wa kuamkia leo kwa shamrashamra mbalimbali.
Katika michezo hiyo, China imejizolea medali 239, ikifuatiwa na Uingereza 147, na ya tatu ni Ukraine 117.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, Kenya inaongoza kwa kubeba jumla ya medali 6 na Uganda Medali 1.
18 September, 2016
Download Audio Mpya Kutoka kwa Diamond Plutnum Ft Raymond - Salome
Bofya DOWNLOAD hapo chini Kuupakua wimbo Huo. DOWNLOAD pia na Club Banngers Version hapo chini
Subscribe to:
Posts (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
Mpenzi msomaji wa safu hii ni siku nyingine tunakutana katika kujuzana,kukumbushana, na kuelimishana mila na desturi za makabila mbalimbal...
-
This is a song sang by a very gifted woman Adele, I sang it to show world that everyone appreciate and love to enjoy good music! Asa...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...

