30 August, 2016

Arsenal kumtoa Jack Wilshere kwa mkopo

Kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Jack Wilshere
Arsenal iko tayari kumtoa kwa mkopo kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere ili kupata fursa ya kujumuika katika kikosi cha kwanza cha timu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24,ambaye mchezo wake uliathirika kutokana na jeraha la mguu aliichezea Arsenal mara tatu pekee msimu uliopita baada ya kupata jeraha hilo.
Aliichezea Uingereza mara sita pekee msimu ulioipita ,ikiwemo mechi tatu katika mashindano ya Euro2016, lakini hakuchaguliwa katika kikosi cha kwanza cha mkufunzi Sam Allardyce wiki hii.
Arsenal ililipa pauni milioni 35 kumnunua mchezaji wa Switzerland Granit Xhaka msimu huu

Kampuni ya Apple kulipa kodi iliokwepa Ireland

Kampuni ya teknolojia ya Apple

Tume ya Ulaya inatarajiwa kuamrisha kampuni kubwa ya teknolojia ya Apple kulipa mabilioni ya dola kama kodi iliyokwepa kulipa.
Hii inafuatia uchunguzi uliofanywa kubainisha makubaliano kuhusu kodi kati ya kampuni hiyo na serikali ya Ireland.
Tume ya Ulaya imewalalamikia mawaziri wa Ireland kwa kuipa Apple kandarasi inayoondoa kodi kwa makubaliano ya kutoa ajira kwa raia wa nchi hiyo.
Apple imesisitiza kwamba hakukua na muafaka maalum, na kwamba inalipa kodi kubwa nchini Marekani ambapo makao yake makuu yapo.
Kampuni ya Apple ni moja ya mashirika ya Marekani yanayolengwa na Tume ya Ulaya kutokana na mikataba yake ya kodi.

Mcheza filamu za vichekesho Gene Wilder afariki

Mcheza filamu Gene Wilder afariki dunia
Mcheza filamu za vichekesho nchini Marekani, Gene Wilder amefariki dunia akiwa na miaka 83.
Wilder amekua akiugua ugonjwa kwa kukosa fahamu{ Alzheimers}.
Aliwahi kucheza filamu maarufu ya , ''Willy Wonka-The Chocolate Factory''.


29 August, 2016

Hivi ndivyo ilivyokuwa red carpet ya MTV Video Music Awards 2016


Usiku wa August 28 ulikua ni usiku ambao tuzo kubwa ulimwenguni  MTV Video Music Awards zilikua zikitolewa. Hafla ya Tuzo hizo ilifanyika katika jiji la New York nchini Marekani. Wasanii wakubwa nchini marekani walihudhuria katika shereha za Utoaji wa tozo hizo. Baadhi wa wasanii walio tekelezea pande hizo ni Kanye West na Mkewe Kim-Kardashian, Meek-Mill na Mpenziwe Nick Minaj, Beyonce na Mwanawe Blue Eve na wengine kibao kama utakvyo waona hapo kwenye picha chini.
vma-arrivals-2016-1 vma-arrivals-2016-2 vma-arrivals-2016-3 vma-arrivals-2016-4 vma-arrivals-2016-5 vma-arrivals-2016-6 vma-arrivals-2016-7 vma-arrivals-2016-8 vma-arrivals-2016-9 vma-arrivals-2016-10 vma-arrivals-2016-11 vma-arrivals-2016-12 vma-arrivals-2016-13 vma-arrivals-2016-14 vma-arrivals-2016-15 vma-arrivals-2016-16 vma-arrivals-2016-17 vma-arrivals-2016-18 vma-arrivals-2016-19 vma-arrivals-2016-20 vma-arrivals-2016-21 vma-arrivals-2016-22 vma-arrivals-2016-23 vma-arrivals-2016-24 vma-arrivals-2016-25 vma-arrivals-2016-26 vma-arrivals-2016-27 vma-arrivals-2016-29

NA HIVI NDIVYO RIHANA ALIVYO PERFORM KATIKA JUKWAA LA MTV VIDEO MUSIC AWARDS.

video mpya ya Chris Brown ‘Grass Ain’t Greener’

Chriss Brown anazidi kufanya poa katika game maana kila baada ya ngoma hutoa ngoma kali zaidi. Ni mida mchache tuu umepita baada ya kuchia Audio ya ngoma hii  ‘Grass Ain’t Greener’, Chriss kaachia Video ya ngoma hii. Tizama hapo chini kisha washirikishe wana kitaaa.

Wanasayansi wanasema maji ya dunia yanahama

Ramani ya dunia
Wanasayansi wametumia picha za za setilaiti kuchunguza namna maji ya dunia yalivyohama kwa zaidi ya miaka 30. 

Walibaini kwamba kilo mita za mraba 115,000 za ardhini kwa sasa zimefunikwa na maji na kilomita 173,000 za maji zimefunikwa sasa na ardhi.
Ongezeko kubwa la maji limetokea katika eneo tambarare la betan , huku bahari ya Aral eneo kubwa la maji sasa limegeuka kuwa ardhi.
wanasayansi hao wanasema kuwa maeneo ya mwambao pia yamekuwa na mabadiliko makubwa .
Utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Deltares ya nchini Uholanzi umechapishwa na jarida la mabadiliko ya asili ya hali ya hewa. Tibetan Plateau
Watafiti walitathmini picha za setilaiti azilizochukuliwa na kituo cha wataalam wa masuala ya anga cha Nasa ,ambacho kimekuwa kikichunguza dunia kwa miongo kadhaa .
Waliweza kufuatilia mabadiliko ya sehemu ya juu ya dunia inayoweza kuonekana kwenye kipimo maalum .
Waliweza kubaini eneo pana ambalo wakati mmoja liliwahi kuwa ardhi ambalo sasa limekuwa na maji , eneo kubwa zaidi likiwa ni lile la maeneo tambarare yenye vilima ya Tibetambako barafu zilizoyeyuka zinasababisha maziwa makubwa .Korea kaskazini
Kuongezeka kwa idadi ya mabwawa pia kunaongeza kiwango cha maji, na kwa kutumia data za setilaiti , Timu hiyo ya wanasayansi iliweza kugundua shughuli za ujenzi ambazo hazikuripotiwa awali.
Dr Fedor Baart kutoka taasisi ya Deltares anasema : "Tulianza kuangalia kwenye maeneo ambayo hayakuwekwa kwenye ramani awali.
"Tulifahamu nchini Myanmar kwamba mabwawa kadhaa yalikuwa yanajengwa, lakini tuliweza kuona mengi . Na pia tuliweza kuona Korea kaskazini na tukaona mabwawa yanayojengwa huko karibu tu na mpaka wa Korea Kusini." bahari ya Aral
Vile vile watafiti waliweza kubaini kwamba hata maeneo makubwa ya maji yamebadilika kuwa ardhi sasa
Mabadiliko haya makubwa yalionekana katika bahari ya Aral Sea katika Asia ya kati.
Yale yaliyowahi wakati mmoja kuwa maziwa makubwa duniani kwa sasa karibu yanakauka kabisa baada ya wahandisi kuelekeza maji katika shughuli za kilimo cha umwagiliaji.

CHANZO: BBC 

Joao Mario ajiunga na Inter Milan

Joao Mario

Joao Mario amejiunga na klabu ya Inter Milan kutoka Sporting lisbon kwa kitita cha pauni milioni 38.4 na kuwa mchezaji ghali zaidi wa Ureno kuwahi kuuzwa na klabu ya Ureno.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliyashinda mauzo ya Cristiano Ronaldo ya pauni milioni milioni 12.24 na Nani aliyeuzwa kwa kitita cha pauni milioni 25 kuelekea Manchester United.
Inter bado inaendelea na mazungumzo ya kumsajili Gabriel Barbosa kutoka Santos.
Kiungo wa katiu Mario aliichezea Sporting mara 171 na kushinda Euro 2016 na Ureno.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...