29 August, 2016

Joao Mario ajiunga na Inter Milan

Joao Mario

Joao Mario amejiunga na klabu ya Inter Milan kutoka Sporting lisbon kwa kitita cha pauni milioni 38.4 na kuwa mchezaji ghali zaidi wa Ureno kuwahi kuuzwa na klabu ya Ureno.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliyashinda mauzo ya Cristiano Ronaldo ya pauni milioni milioni 12.24 na Nani aliyeuzwa kwa kitita cha pauni milioni 25 kuelekea Manchester United.
Inter bado inaendelea na mazungumzo ya kumsajili Gabriel Barbosa kutoka Santos.
Kiungo wa katiu Mario aliichezea Sporting mara 171 na kushinda Euro 2016 na Ureno.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...