17 January, 2016

Man United yailaza liverpool


Wayne Rooney alifunga bao lake la kwanza katika uwanja wa Anfield tangu mwaka 2005 na kuiwezesha timu yake kupanda katika jedwali la ligi ya Uingereza.
Liverpool ilitawala mchezo huo huku mkwaju wa Emre Can ukipanguliwa na kipa David De Gea.
Lakini Liverpool walilazimika kulipa makosa yao wakati Wayne Rooney alipofunga mkwaju mzuri akiwa karibu na eneo la hatari baada ya kichwa cha Marouane Fellaini kugonga mwamba wa goli.
Wageni hao ambao sasa wako katika nafasi ya tano walikuwa hawajashambulia hata mkwaju mmoja katika lango la Liverpool hadi mshambuliaji huyo wa Uingereza alipofunga bao hilo la ushindi.
Liverpool itasalia katika nafasi ya tisa ikiwa alama sita nyuma ya Manchester United.

Video: Barakah Da Prince - 'Siwezi'

post-feature-imageSiwezi is a new hit video directed by super dupa Kenyan director Kevin Bosco Jr, was shot at Runda area in Nairobi Kenya. Audio was produced by Bob Manecky at AM Records in Dar es Salaam, Tanzania.

Huu hapa msimamo ligi kuu Spain

Image result for la liga
PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Atletico de Madrid1914232781944
2Barcelona18133244152942
3Real Madrid19124352183440
4Villarreal20124426161040
5Celta de Vigo2010463230234
6Sevilla209562822632
7Eibar198652720730
8Athletic Club198472722528
9Deportivo de La Coruna2061042724328
10Malaga206681517-224
11Valencia CF195862319423
12Getafe196582127-623
13Real Sociedad205692328-521
14Espanyol1963101730-1321
15Real Betis205691328-1521
16Las Palmas194691927-818
17Granada CF1945102036-1617
18Sporting de Gijon1843111629-1315
19Rayo Vallecano1943122143-2215
20Levante2035121736-1914

GABON NA MOROCCO HAKUNA MBABE CHAN 2016,

Kiungo wa Gabon, Rodrigue Moundougua (kulia) akijaribu kumpita beki wa Morocco, Abdessalam Benjelloun katika mchezo wa Kundi A Michuano ya Ubingwa wa Mataifa wa Afrika (CHAN) Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda usiku wa leo. Timu hizo zimetoka 0-0.
Rwanda iliyoshinda mchezo wa kwanza jioni 1-0 dhidi ya Ivory Coast sasa inaongoza Kundi A. 


SIMBA YAITULIZA MTIBWA SUGAR NA KUNG’ANG’ANIA NAFASI YA TATU

Mchezaji wa Simba akipata hug la nguvu kwa kocha wa Mtibwa baada ya mechi yao kumalizika
Jumamosi ya January 16, 2016 ulipigwa mchewzo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Simba SC ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo dhidi ya Mibwa Sugar watoto wa Manungu-Turiani, Morogoro mchezo ambao ulimalizika kwa Simba kufanikiwa kulipa kisasi kwa Mtibwa Sugar kwa kuitungua bao 1-0 bao ambalo Simba walifungwa kwenye michuano ya Mapinzuzi na kutupwa nje ya michuano hiyo wiki iliyopita kwenye visiwa vya marashi ya Karafuu Zanzibar.
Bao hilo likaipa Simba fursa ya kuendelea kusalia katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi nyuma ya watani zao Yanga ambao wako nafasi ya pili kuhu leo wakishuka dimbani kutafuta pointi tatu muhimu wakati vinara wa ligi hiyo Azam FC wenyewe jana walibabwa koo na vibonde African Sports na kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo uliochezwa usiku kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Hapa kuna picha kadhaa ambazo zinakupa fursa wewe msomaji kuangalia baadhi ya matukio muhimu yaliyojiri kwenye game ya Simba vs Mtibwa.DSCF1374
Ajib na Baba Ubaya wakiwania mpiraKocha wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime akimpa mpira beki wa kulia wa Simba Emiry Nimuboma Simba-MtibwaAjib na Baba Ubaya wakiwania mpiraWachezaji wa Simba Amis Kiiza (kushoto), Peter Mwalyanzi (katikati) na Ibrahim Ajib (kulia) wakishangil;ia bao lilipachikwa wavuni na Kiiza

Rais wa Burkina Faso amesema takriban watu 21 wameuwawa katika shambulio kwenye hoteli moja mjini Ogadugu na wanamgambo waliovamia hotel hiyo.

Roch Mark Christian Kabore amesema washambuliaji wanne waliovamia hotel hiyo waliuliwa ambapo wawili kati yao ni wanawake. Shambulio hilo lililotokea kwenye hotel ya Splendide kwenye mji mkuu wa Ouagadougou sasa limemalizwa.
Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo amesema wanamgambo hao wameuwa watu kumi na nane kutoka mataifa mbalimbali. Zaidi ya watu mia moja na ishirini walikimbia hotel hiyo maarufu kwa watalii.
walionusurika wanasema wanamgambo hao walianza kupiga risasi kwenye jengo hilo na kisha kuliwasha motoKundi la Kigaidi la Al Qaeda kwenye ukingo eneo jangwa imesema lina husika na shambulio hilo.
Watu 126 waliokuwa mateka waliachiliwa huru katika hoteli ya Splendid iliopo katika mji mkuu wa taifa hilo la Magharibi mwa Afrika Ouagadougou, kwa mujibu wa waziri wa maswala ya ndani.
Wapiganaji wanne waliuawa aliongezea huku watu 21 wa mataifa 18 tofauti wakifariki wakati wa shambulio ambalo pia liliulenga mgahawa huo.
Vikosi maalum vya Ufaransa vinasaidia wanajeshi wa taifa hilo katika oparesheni hiyo.Mnamo mwezi Novemba shambulio la AQIM katika hoteli moja ya Bamako nchini Mali liliwauwa watu 19.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya Januari 17

Kutana na habari zilizopo katika magazeti pendwa hapa nchini yakiwa yame beba habari zote kwa ujumla.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...