17 January, 2016

SIMBA YAITULIZA MTIBWA SUGAR NA KUNG’ANG’ANIA NAFASI YA TATU

Mchezaji wa Simba akipata hug la nguvu kwa kocha wa Mtibwa baada ya mechi yao kumalizika
Jumamosi ya January 16, 2016 ulipigwa mchewzo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Simba SC ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo dhidi ya Mibwa Sugar watoto wa Manungu-Turiani, Morogoro mchezo ambao ulimalizika kwa Simba kufanikiwa kulipa kisasi kwa Mtibwa Sugar kwa kuitungua bao 1-0 bao ambalo Simba walifungwa kwenye michuano ya Mapinzuzi na kutupwa nje ya michuano hiyo wiki iliyopita kwenye visiwa vya marashi ya Karafuu Zanzibar.
Bao hilo likaipa Simba fursa ya kuendelea kusalia katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi nyuma ya watani zao Yanga ambao wako nafasi ya pili kuhu leo wakishuka dimbani kutafuta pointi tatu muhimu wakati vinara wa ligi hiyo Azam FC wenyewe jana walibabwa koo na vibonde African Sports na kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo uliochezwa usiku kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Hapa kuna picha kadhaa ambazo zinakupa fursa wewe msomaji kuangalia baadhi ya matukio muhimu yaliyojiri kwenye game ya Simba vs Mtibwa.DSCF1374
Ajib na Baba Ubaya wakiwania mpiraKocha wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime akimpa mpira beki wa kulia wa Simba Emiry Nimuboma Simba-MtibwaAjib na Baba Ubaya wakiwania mpiraWachezaji wa Simba Amis Kiiza (kushoto), Peter Mwalyanzi (katikati) na Ibrahim Ajib (kulia) wakishangil;ia bao lilipachikwa wavuni na Kiiza

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...