Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo amesema wanamgambo hao wameuwa watu kumi na nane kutoka mataifa mbalimbali. Zaidi ya watu mia moja na ishirini walikimbia hotel hiyo maarufu kwa watalii.
walionusurika wanasema wanamgambo hao walianza kupiga risasi kwenye jengo hilo na kisha kuliwasha moto
Watu 126 waliokuwa mateka waliachiliwa huru katika hoteli ya Splendid iliopo katika mji mkuu wa taifa hilo la Magharibi mwa Afrika Ouagadougou, kwa mujibu wa waziri wa maswala ya ndani.
Wapiganaji wanne waliuawa aliongezea huku watu 21 wa mataifa 18 tofauti wakifariki wakati wa shambulio ambalo pia liliulenga mgahawa huo.
Vikosi maalum vya Ufaransa vinasaidia wanajeshi wa taifa hilo katika oparesheni hiyo.
No comments:
Post a Comment