07 July, 2015

Sababu sita usizotaka kuzijua kwanini bado upo single….

Sio kila mtu anataka kua katika mahusiano kitu ambacho ni sawa kwa asilimia 100.Lakini kuna watu ambao kila saa wanalalamika kwa kua wapo single japokua hawajahi kujaribu kutatua naweza kusema tatizo hili. Kuna watu inawezekana ni kweli hawajakutana na watu sahihi wa kuwa nao lakini kunawengine huamua kuwa wa kweli kueleza ni sababu gani wapo single.
1 . Unajibana mwenyewe na vigezo na viwango fulani
Utasikia jamaa anasema mimi nataka demu mwenye umbo zuri kama Kim Kardashian , sasa jiulize hawa watu wako wangapi na hata kama wapo wengi hua wana wanaume kibao wanawafukuzia. Au kwa upande wa wadada utasikia nataka mtu mwenye gari , awe na nyumba , awe msomi , analipwa mshahara wa kutosha kunitoa kila weekend. Watu wanaweza kukushangaza   lakini hawawezi kama utawageuzia migongo na kutowapa nafasi. Haya ni mahesabu tu, kama ukiweka vigezo na viwango kibao vya jinsi unavyotaka  mpenzi wako aweje utabakia na watu 10 tu duniani wanaoweza kua hivyo na wewe utakua ni mpumbavu sababu umejitengenezea mtu wa kusadikika na unastahili kuwa single.kubali kwamba hauelewi chochote kinachoendelea baina yako na mtu fulani na vingine vitakuja kawaida tu. Zingatia kukutana na watu halisi , jifunze na upate kuwajua , na upime kama unaendana nao kama watu halisi na sio watu wa kufikirika ambao hata kama wapo inawezekana wasikutake wala kukupenda. Inauma lakini ndio ukweli halisi.
Relationship-Wamegombana-hawa
2. Kama unataka bora  inabidi na wewe uwe bora
Watu wanajipenda ambacho ni kitu cha kawaida kabisa na wanafikiria kwamba wanaitaji mtu bora katika maisha yao lakini jiulize ili upate mtu aliye bora haufikiri kwamba inabidi uweze kukidhi ubora wa mtu huyu unayemtaka ? Unaposema nataka mtu mrefu , anayelipwa mshahara wa mamilioni,anayependa watu, mwenye nyumba nzuri na gari zuri , anayeweza kulea watoto , je ni kitu gani ambacho na wewe utakiongeza kwenye uhusiano wako na mtu huyu? Uhusiano sio “One-way Street” kawa watasha wanavyosemaga.Si maanishi kwamba inabidi uwe bora kabisa , hapana sema ni muhimu kujitathmini mwenyewe na kuangalia ni kitu gani unaweza kuchangia kama ukimpata mtu fulani. Wakati upo single una muda mwingi wa kujifunza kuhusu wewe , sio lazima uwe bora lakini unaweza kufanya vitu vidogovidogo  kama kua msikilizaji mzuri wa maongezi , kujifunza mambo unayopenda kufanya na kadhalika.
Relationship-wapenzi-wanachuniana-kitandani
3. Unajipenda Sana
Ushawahi kuona watu wanaojiona kama Dhahabu , watu kama hawa hata siku moja hawawezi kukubali kama wamekosea sehemu au wamefanya kitu kibaya kwasababu wanajipenda sana na kujiona kwamba wao ndio bora kuliko wengine. Kuna mda inabidi uamke usingizini na ujitambue kwamba wewe sio bora na kwamba inabidi utoe ili upokee.  kwa mfano kama wewe demu unajijali sana na unategemea mwanaume akufukuzie , akutafute kila saa , aonyeshe dalili zote kwamba anakupenda wakati wewe unamwangalia tu labda utakua hauko tayari kupenda na kujali kama watu wafanyavyo kwenye mwanzo wa mahusiano.Sio kila saa ni kuhusu unachotaka kwani ni wakati muafaka wa kuanza kujali na kusikiliza upande wa pili unataka nini.Watu hua wanajua kama mtu anajisikia , kama mtu anategemea kuabudiwa na ni kitu ambacho hakivutii kabisa.
Relationship-woman-at-bar
4. Unajifungia ndani
Kuna watu wanajifungia ndani alafu wanapigia watu makelele kwamba wapo single,sijui wanataka story kama ya cinderella. Kwa watu hawa inabidi waamke. Kama unataka kuwa na mtu usitegemee atadondoka tu kutoka popote.Yes, unaweza hotea lakini ukweli ni kwamba upo katika hatihati ya kuishi peke yako maisha yako yote.Najua kutoka na kujichanganya ni vigumu hasa kwa wale watu ambao hawapo “Comfortable”  jinsi walivyo.Kutoswa inaogopesha na inauma.Lakini unajua kitu gani hakiumi? ni kujua kwamba umejaribu na umeweka juhudi zako zote . Kuamini kitu unachotaka ni muhimu na  kukitafuta pia.Toka nje, kutana na watu , sio tu bar bali hata kwenye vitu mbalimbali  kama movies hivi au swimming kutokana na “hobby” yako. Kama vyote umeshindwa na bado unataka kujifungia ndani basi fanya hata “online dating” , siku hizi kuna app ya simu inaitwa tinder ina watoto kibao wazuri wa kibongo.
Relationship-Amelala
5. Haujielewi unataka nini
Hii ni muhimu sana , kama upo tayari kuwa serious katika mahusiano basi uwe tayari kuwa serious. Kama ukikutana na mtu akaanza kusema maneno kaka ” Sitafuti kitu serious kwa muda huu” au “Sijielewi bado ninataka nini”  basi usijidanganye na kusema ” Sawa tu , ngoja tuone mambo yataendaje” kwani utaishia pabaya na mwisho wake kutofanikisha malengo yako.
Relationship-wapenzi-wanagombana-beach
6. Sio mvumilivu na unakata tamaa kirahisi
labda ushajiweka mara kibao kwa wadau au umekuwa na dates mbaya nyingi au haujajibiwa message zako. Kwa sababu fulani fulani watu wengine hnyoosha mikono juu na kusema “Yamenishinda, hamna haja” , lakini ukweli ni kwamba sio kila mtu utakayekutana naye inabidi awe bora tena ni jambo la kheri umefikiria hivyo. kwahiyo fanya kila majaribio kama sehemu ya kupata ujuzi zaidi.Relationship-Giving-Up

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...