25 June, 2015

Epuka mawazo hasi kwa mwenzi wako, ni ugonjwa wa moyo

Taarifa kwako msomaji wangu ni kuwa kuna watu wengi wameachana kwa sababu ya kuwa na mawazo hasi juu ya wenzi wao. Hakuna imani kati yao. Iwe mmoja anamtuhumu mwenzake au wote ni kama Pwagu na Pwaguzi.Zipo hisia zinazowaongoza wanaume wengi kuhusu wanawake. Hawataki wafanye kazi, ikibidi wakae tu nyumbani kwa hoja kuwa wanapokuwa maofisini wataanzisha uhusiano mpya na
wafanyakazi wenzao au kwenye mapito ya kazi zao.

Wale wanaoruhusu wake zao wafanye kazi, kila siku roho juu. Macho pima kwenye simu za wenzi wao. Hawana imani ya asilimia 100 kwamba siku hupita bila kusalitiwa. Wanateswa na sononeko la moyo. Pengine mwenzake ni mwaminifu lakini wasiwasi wa mapenzi ndiyo ugonjwa wa moyo

Haipendezi kumfikiria mwenzako kwa ubaya. Inashauriwa umuamini na ujiamini. Mawazo chakavu kuhusu mwenzi wako ni sumu. Ukiyaendekeza yanaweza kukufanya ushindwe kutekeleza mambo ya msingi.

Mwanamuziki Stara Thomas amelifafanua hilo vizuri kwenye wimbo wake  wa Wasiwasi wa Mapenzi.  Kwamba mtu anaweza kujawa na hofu ya kusalitiwa na mwenzi wake mpaka roho ikawa juu juu. Kumbe siyo kweli hata kidogo.

Unaweza kumvaa mtu asiye na hatia na kugombana naye kwa sababu tu ya mawazo kwamba anakuchukulia mali yako. Siku zinasogea, baadaye unakuja kugundua kuwa hisia ndizo zilikupeleka ndivyo sivyo.

Busara za kisaikolojia zinakutaka uwe huru, kwa maana unatakiwa ujiepushe na mawazo mabaya. Mtu akipiga simu ya mwenzi wako, usikurupuke na kuanzisha songombingo, hebu vaa utulivu na upate ufumbuzi kwa njia yenye nidhamu.

Kushika simu ya mwenzi wako na kukagua simu zinazoingia na kutoka ni alama ya kutoamuamini. Ingekuwa humtilii shaka yoyote, usingethubutu kukiganda ‘kiselula’ chake. Hujui tu, unamdhalilisha kwa kumuona hajatulia.

Unataka kuona SMS zinazoingia na kutoka. Hulali mpaka uone simu alizopiga na alizopigiwa. Presha hiyo yote ya nini? Jaribu kumuamini na umuoneshe jinsi usivyo na shaka naye. Mwache yeye mwenyewe atumie vibaya imani yako kwake.
Kuna mtu kwa wasiwasi alikuwa anashindwa kutimiza majukumu yake ya kila siku, badala yake anakwenda kujificha nje ya ofisi ya mke wake, anashinda pale, lengo ni kuona wakati wa ‘lunch’ mkewe anaongozana na nani.

Ikiwa siku hiyo mkewe kaongozana na mfanyakazi mwenzake wa kiume kwenda lunch, jioni nyumbani ni kesi. “Nimepata taarifa zako, leo ulikwenda lunch na mwanaume, yule ni nani?” Hana lolote, hajaambiwa na yeyote, ni yeye mwenyewe na upekupeku wake.

UNAMKOSEA HESHIMA MWENZI WAKO
Iwe hutaki mwenzi wako afanye kazi au unamsumbua kwa namna yoyote ile, jawabu ni moja tu kwamba humheshimu. Kutokuwa na imani na yeye, maana yake ndani yako kuna hisia kuwa hajatulia. Ni malaya au kicheche kwa lugha ya mtaani.

Je, unadhani ni vema kumuona mwenzi wako hajatulia? Kama ndivyo, unaendelea kuwa naye kwa sababu gani? Asipoheshimiwa na wewe, unataka nani mwingine ampe heshima?

Mwenzi wako anapogundua kuwa humheshimu, taratibu naye atakushusha thamani. Akigundua huna imani naye, atakosa raha. Hata kama anakustahi leo, ipo siku ataona hana sababu ya kuendelea na wewe.

Mwingine anahaha kuulizia nyendo za mwenzi wake kwa marafiki. Hilo ni kosa kubwa kwa sababu huyo unayemuuliza, mwisho anaondoka na kitu kikubwa kwamba hakuna uaminifu kwenye uhusiano wako.

Kuna mtu ambaye huweka mabodigadi wa kufuatilia nyendo za mke wake kila anapokwenda. Anayedhani kufanya hivyo ni dawa, ameula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua. Anakosea kupita kiasi.
[next]

Watu wenye mawazo mabaya juu ya wapenzi wao mara nyingi wanakuwa na misukumo ya kufanya uamuzi ambao siyo sahihi. Yupo anayeweza kukatisha shughuli zake za siku kwa ajili ya kumfuatilia mwenzake.

Mwingine anahaha kuulizia nyendo za mwenzi wake kwa marafiki. Hilo ni kosa kubwa kwa sababu huyo unayemuuliza, mwisho anaondoka na kitu kikubwa kwamba hakuna uaminifu kwenye uhusiano wako.

 Kuna mtu ambaye huweka mabodigadi wa kufuatilia nyendo za mke wake kila anapokwenda. Anayedhani kufanya hivyo ni dawa, ameula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua. Anakosea kupita kiasi.

Kumuwekea mwenzi wako bodigadi ni sawa na kumtoa sadaka. Kama hujui, basi wapo wenzako leo hii wanalia kwa kusaga meno. Kiherehere chao kiliwaponza. Binadamu hafugwi kama kuku wa kisasa.

Wapo wengi ambao walipowaweka mabodigadi, ikawa ni kama wamerahisisha maisha. Wenzi wao wakatoka na hao hao mabodigadi. Kwa mwenye mali inakuwa ngumu zaidi kujua. Bodigadi atajitaja?

Bila shaka haiwezekani. Hii ina maana kuwa bodigadi ataendelea ‘kula’ chakula cha bosi wake bila mhusika mwenyewe kujua. Mwenye mali akingoja aambiwe mwizi ni nani, kumbe kikulacho kipo nguoni mwake.

Siku anagundua inakuwa kilio na majuto. Haitasaidia, kwani majuto ni mjukuu! Ulisikia jinsi mke wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Nompumelelo Ntuli alivyopewa mimba na bodigadi wake wa Ikulu. Yanatokea na yapo.

Ni wivu lakini huu ni ule ambao huzidi hisia za ndani. Ukikaa peke yako unakosa amani kwa kudhani kuwa kule ambako mwenzi wako yupo, atakuwa anakusaliti kwa mwanaume/mwanamke mwingine.

MTAGOMBANA KILA SIKU
Ukiachana na pointi hiyo kwamba anaweza kukusaliti, kubwa zaidi ni jinsi ambavyo uhusiano wenu unavyoweza kuingia kwenye misukosuko ya mara kwa mara. Wasioaminiana, hawawezi kupitisha wiki bila ugomvi.

Mwenzi wako akichelewa kurudi nyumbani, jambo la kwanza utashikwa na wasiwasi. Hautakuwa wasiwasi wenye maumivu ya hofu kwamba pengine yupo kwenye matatizo, la hasha!
Si ajabu hapo ulipo utavuta picha kwamba yupo kitandani na mtu mwingine kwenye nyumba ya kulala wageni, wote wawili hawana nguo hata moja. Ukifumba macho unaona ‘live’. Kichaa kinazidi kukupanda.

Akirudi nyumbani, badala ya kumuuliza za huko atokako, utamvaa huku kifua chako kikiwa kimejaa jazba. Atakalokujibu hutalielewa kwa maana ndani ya ubongo unamfikiria vibaya na umeshamjaza tuhuma nyingi.

Maskini wa Mungu, kumbe mwenzake alicheleweshwa na foleni za njiani. Inawezekana kazi za siku hiyo zilikuwa nyingi kuliko kawaida. Pengine ofisini kwake kulikuwa na wageni ambao walimfanya ashindwe kutoka kwa wakati muafaka.

Endapo atakujibu ukweli alionao lakini wewe ukawa unasisitiza ugomvi, mwisho mtagombana kweli. Baadaye ataona kama noma na iwe noma, hivyo ukipanda naye atakupandishia. Mapenzi hayapo hivyo.

Kuna faida kubwa unapomuamini mwenzi wako. Busara zikuongoze kuwa mtulivu. Hata kama anakusaliti, hutakiwi kupandisha mizuka na kumwaga tuhuma zisizo na uthibitisho, vaa hekima kukusanya ushahidi.

Ni kosa kubwa kuishi na mwenzi wako kwa mtindo wa kuwindana. Kwamba ndani ya ubongo wako unaamini anakusaliti, kwa hiyo unamtega aingie kwenye 18 zako muachane. Huo ni uhusiano ambao hauwezi kuwa na furaha.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...