19 April, 2016

Sababu tano ni kwa nini Bongo flava ya Awali ilikuwa bora kuliko ya bongo Flava ya Sasa

Leo nmepanda tena hapa Mtokambali nikiwa upande mmoja na upande huo siyo mwingine bali ni ule upande wa ile bongo flava ya P-FUNK MAJANI, MWIKA MWAMBA, MJ na wakali wote waliowahi kukipia vyema katika game hii ya Bongo flava kipindi cha nyuma.Yawezekana kwa namna moja ama nyingine ukajiuliza ni kwa nini nmeamua upande hou angali Bongo flava ya sasa inaonekana kufanya vyema!

Ngoja nikupe sababu ni kwa nini nasema hivyo:-
1.Vipaji halisia vilikua huku.
Ifahamike kua sjasema wasanii wa sasa hawana vipaji laa hasha, ninaposema vipaji vya kweli vilikua kipindi cha nyuma namaanisha kuwa ubunifu wa hali ya juu ulionekana zaidi kuliko sasa, ukitaka kujua ukweli juu ya hili chukua ngoma Moja ya Bongo Flava iliyotengenezwa miaka ya 2000-2005 na uchukue ngoma ya sasa ilofanywa kuanzia 2010-016 utatambua ni kwa nini nmeitaja sababu hii.

2.Hamasa ya kweli
Kama wewe ni mpenzi wa burudani ya muziki hapa nyumbani kuanzia miaka ya 1998-2007 utakua unafahamu nachotaka kukielezea hapa, Hamasa ya kweli ilipatikana katika muziki huu sababu nyimbo zilizokua zikitungwa wakati huo zilikua zimejaa ujumbe na mafunzo tele kwa jamii na hivyo watu weengi walihamasika vilivyo (mimi ni mmoja wa hao tulio hamasika). Chukulia nyimbo kama ELIMU DUNIA, aloimba Daz-Baba, au ile ya NDIO MZEE aliyoimba Prof J na ngoma nyiingi amabazo zilikimbiza wakati ule utaona ni jinsi tulivyo pata darasa huru.

3.Production ya kweli.
Hapa nitazungumzia studio zilizokua zikitumika kurekodi ngoma hizo mfano Bongo Records, Mj, na 41 records. Hakika maproducer waliokua wakifanya kazi katika studio hizo walikua na vipaji vya hali ya juu kiasi kwamba ilikua ni vugumu msanii kukubaliwa kuingia studio moja kwa moja nakurekod bila kusota kweli na kuiva kweli kweli. Midundo (Kicks na snare)  vilikua hatari na unique. Mkono wa Producer kama Majani ulikua umebarikiwa kweli kweli na ilikua huwezi kufananisha mkono wa Majani na Mkono wa producer yeyote yule, kila mmoja alikua na ladha yake. Lakini bongo flava ya leo ni mwendo wa kukopi na kupaste tuu hakuna ubunifu.

4.Ushirikiano ulikuwako.
Jiulize ni kwa nini mwanzoni kulikuwako na makundi meengi ya muziki na yalifanya poa mno ila kwa sasa makundi hayo siku hizi hayapo na kama yakijitokeza baada ya muda mchache utasikia kundi hilo limevunjika? huu ni ushahidi tosha kua ushirikiano kwenye game la bongo flava ya sasa hakuna kabisa na ndio maana utamu wa muziki huo unazidi kupotea.

5.Muziki ulijulikana kama kipaji na sio biashara.
Hapa ndipo utabisha na kuniambia UTANDAWAZI umechangia muziki wa sasa kuonekana biashara, Kama ndio hivyo jiulize ni kwa nini kuku wa kienyeji anauzwa ghali kuliko wa kisasa? Jibu utakalokuwa nalo utaniachia kwenye comment hapo chini ila kwa sasa acha nikuambie kuwa wasanii wa hapo nyuma walifanya muziki for funy na sio kwa ajili ya biashara licha ya kuonekana wakikazana na kuuza album kwa wahindi nakujipatia kipato kidogo ila wao waliwekeza nguvu kubwa kaktika kukuza vipaji vyao maana waliamini kizuri kitajiuza na kibaya kitajitembeza.

Basi hizo ni sababu Tano(5) ni kwa nini bongo flava ya Mwazo ni bora kuliko hii ya sasa. Tukutane tena panapo majaliwa Hapa hapa MTOKAMBALI.

Ningependa uniachie maoni yako hapo chini kwenye comment box na kama una jambo lakunieleza kuhusiana na makala hii ama una swali lolote kuhusiana na makala hii niulize nitakujibu mara moja kwa kadri niwezavyo.
Tangazo

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...