29 January, 2016

De Bruyne kukaa nje wiki sita


Kiungo wa Manchester City, Kevin de Bruyne, atakua nje ya dimba kwa muda wa wiki sita baada ya kuumia goti siku ya Jumatano.
De Bruyne aliumia goti la kulia katika mchezo kombe la Capital, ambapo Man City, waliwakabali Everton, na kushinda kwa mabao 3-1.
Wakala wa mchezaji huyu Patrick de Koster, amesema" Nimezungumza na Kevin, amesema atarudi uwanja kwa nguvu zaidi."
Mchezaji huya atakosa michezo muhimu ya timu yake ukiwemo ule wa fainali ya kombe la Capital, dhidi ya Liverpool, hapo Februari 28, pia atakosa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi Dynamo Kiev.
Kulikua na wasiwasi huenda nyota huyu asingeweza rudi dimbani mpaka mwisho wa msimu.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...