Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea tena kushika kasi wikiendi hii kwa nyasi za viwanja saba kuwaka moto siku ya jumamosi.
Wagosi
wa kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Yanga, Wekundu wa msimbazi
Simba sport klabu wao watakua wenyeji wa Afrikani Sport mchezo
utaochezwa kwenye uwanja wa taifa Dar Es Salaam.Maafande wa Jkt Ruvu watawaalika wana lizombe Majimaji ya Songea, Tanzania Prison watashuka dimbani kuwakabili Azam FC.
Mtibwa Sugar watacheza na Stand United,huku Mwadui Fc ya Shinyanga watakipiga na majirani zao wa Mwanza Toto Afrikans. Kagera Sugar watapima ubavu na Mbeya City.
Yanga na Azam wanafukuza kileleni wote wakiwa na alama 39, mshambuliaji wa Yanga Amis Tabwe ndie kinara wa kuzipasia nyavu akiwa na mabao 13.
Ligi hiyo itaendelea tena siku ya jumapili kwa mchezo mmoja kuchezwa kwa Mgambo Jkt kucheza na Ndanda FC.
No comments:
Post a Comment